Mishemishe na harakati za Kariakoo na Manzese zilinoga kipekee kwa ‘vibe’ la aina yake jana baada ya timu ya Chrome City kuingia mtaani kuungana na mashujaa halisi wa uchumi wa mijini Tanzania – hustlers. Kuanzia waendesha bodaboda, mama lishe, wauzaji wa nguo, wauzaji wa vifaa vya umeme, mpaka wauza matunda – kampeni hii inawatambua na kusherehekea bidii na jitihada za wapambanaji za kila siku ambazo ni muhimu katika kufanikiwa maishani.

Timu ilifaweza kuzungumza na wapambanaji mbalimbali moja kwa moja kuhusu shughuli zao, burudani na muziki ulioongozwa na ma-DJ wakali hapa nchini, DJ Joozey na DJ Skadi, timu ya Chrome City iliwasikiliza kwa makini ‘hustlers’ wakisimulia ndoto zao, changamoto na mafanikio yao madogo na makubwa na kwa namna gani wanasherehekea na watu waliowashika mkono kufika pale walipo. Ujumbe ulikuwa wazi: Chrome City ni ya Wapambanaji – Kila Mpambanaji Ana Nafasi ya Kusherehekewa na Kuthaminiwa.

Sherehe hii ya hustle itafikia kilele chake Agosti 30 katika Tanganyika Packers, Kawe, wakati wa uzinduzi rasmi wa #ChromeCity. Siku hiyo, hustlers wote – wakubwa kwa wadogo – watakusanyika ili kutambuliwa, kusherehekewa na kuhamasishwa kuendelea kufuata ndoto zao. Uzinduzi huo utapambwa na burudani kali kutoka kwa msanii nyota wa Bongo Flava, D Voice, pamoja na huduma mbalimbali za vinywaji na chakula kwa ajili ya wapambanaji kufurahia siku yao, ndani ya mji wao wa Chrome City.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...