Na Mwandishi wetu, Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kuwezesha wakulima kujikwamua kiuchumi kupitia mikopo yenye riba nafuu.

Ameyasema hayo leo Agosti 1, 2025 jijini Dodoma katika viwanja vya NaneNane alipotembelea Banda la TADB kabla ya kufungua rasmi maonesho hayo Kitaifa.

"Nawapongeza TADB na ninawaelekeza kuendelea kuwafikia watanzania wengi zaidi kwa ajili maendeleo endelevu ya nchi yetu, " alisisitiza Dkt Mpango

Akizungumza namna Benki hiyo inavyokuza uchumi amesema imewezesha vijana, akina mama kujiajiri kwa kupatiwa zana za kilimo zenye ubora na zenye kuleta tija.

Maonesho ya NaneNane Kitaifa yanafanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma Kitaifa na yamefunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...