Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mheshimiwa Tri Yogo Jatmiko amesema Indonesia itaendelea kushirikiana na Tanzania kujengeana uzoefu katika Utafiti wa Kilimo ikiwemo Matumizi ya Teknolojia ya kutengeneza mvua ili kuepuka changamoto za utegemezi wa mvua katika Kilimo.
Balozi Jatmiko amesema hayo Leo Agosti 02, 2025 alipokuwa katika Banda la TARI kwenye maonesho ya Nanenane viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma na kueleza uzoefu wa Indonesia katika matumizi ya Teknolojia hiyo ambayo wamejifunza kutoka Thailand yenye uwezo wa kutengeneza mawingu kuwa mvua pamoja na kupunguza kiwango cha Mvua kubwa zinazonyesha mfululizo na kuathiri shughuli za Kilimo.
Kufikia hatua hiyo amesema kuwa mwaka huu wanategemea kuwa na Mkutano wa wataalamu wa Kilimo hapa nchini ambapo ametambua TARI kama mdau muhimu.
Aidha amesisitiza zaidi kufanya Utafiti katika viungo na vikolezo hasa uzalishaji na uongezaji thamani katika matumizi ya pilipili ambapo ameeleza uwepo wa fursa katika eneo hilo.
Akizungumza kuhusu ushirikiano huo katika Utafiti wa Kilimo, Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dkt Thomas Bwana amesema TARI inashirikiana na Indonesia kwa sasa wanaushirikiano katika zao la Chikichi na nchi hiyo ambayo ni mzalishaji mkubwa wa Chikichi Duniani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...