#MAKINIKIA:
Asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam umeanza mkutano muhimu wa wadau wa sekta ya habari na utangazaji wa Kanda ya Mashariki kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025. Mkutano huu unafanyika katika ukumbi wa PSSSF Commercial Complex, ukiwa na mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi.
Washiriki ni wakuu wa polisi, wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka mikoa yote ya mashariki na Zanzibar.
Katika mkutano huu, watoa mada ni Dkt Egbert Mmoko, Mhadhiri Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano {SJMC), na Mhandisi Andrew Kisaka Meneja Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Wengine ni DCP David Msiime, Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi, Wakili Patrick Kipangula Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) na Dkt. Darius Mukiza mhadhiri SJMC na Bw. Innocent Mungy, Mkuu wa Mawasiliano Serikalini Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC)
Lengo kuu la mkutano ni kuimarisha mshikamano wa wadau wa habari, kuhakikisha weledi, uadilifu na usalama wa taarifa katika kipindi chote cha uchaguzi. Hii ni hatua muhimu ya kuandaa mazingira mazuri kwa vyombo vya habari kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...