Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) wamepata udhamini wa vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 5.5 kutoka kwa Mkurugenzi wa Smart Sport Bw. George Wakuganda, ambaye ni mfanyabiashara wa vifaa vya michezo wa jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa SHIMIWI, Bw. Alex Temba amesema wadhamini hao wametoa jezi, mipira na vikombe kwa ajili ya washindi wa michezo ya mpira wa miguu na netiboli.

Bw. Temba amesema vifaa hivyo vitakuwa msaada mkubwa kwa Shirikisho zimeongeza thamani zaidi kwa kuwa sasa washindi wa michezo ya mpira wa miguu na netiboli watapata jezi tofauti na awali walikuwa wakipata vikombe pekee.

“Kamati ya Utendaji ilipokea ombi la kuja kujitangaza kwenye kikao chetu cha maandalizi ya michezo kule Mwanza na kamati iliomba waidhamini michezo kwa kutoa chochote, basi ametimiza na tumepokea vikombe 20, jezi jozi sita za michezo ya soka na netiboli na mipira ambayo itatumika kwenye mashindano yetu ya mwaka huu 2025 itakayoanza tarehe 1 hadi 16 Septemba huko jijini Mwanza,”

Bw. Wakuganda amesema nia na madhumuni ni kutengeneza mahusiano mazuri na watumishi wa umma, tofauti na sasa mojawapo ya lengo la michezo hii ni kujenga mahusiano baina ya watumishi wenyewe kwa wenyewe.

“Sisi tumeona mashindano ya SHIMIWI yanavipaji vikubwa huenda wengine hawajaviona ila sisi tumeviona, ndio maana tumevutiwa na kutoa msaada kwa kuanzia kwenye michezo hii mikubwa,” amesema Bw. Wakuganda.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...