Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuendeleza ushirikiano katika mapambano dhidi ya Rushwa nchini kupitia ufundishaji wa maudhui ya Rushwa katika Mtaala ulioboreshwa ulioanza kutekelezwa kuanzia Januari 2024.

Hayo yamejiri Agosti 22, 2025 katika ofisi za TAKUKURU Wilaya, Upanga Jijini Dar es Salaam kwenye kikao kazi cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa hati ya makubaliano ya miaka mitano ya mapambano dhidi ya Rushwa iliyosainiwa mwaka 2023.

Akieleza baada ya kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt. Aneth Komba amesema maudhui ya mapambano dhidi ya Rushwa tayari yameingizwa katika Mtaala ulioboreshwa, na wanafunzi wameanza kunufaika na maudhui hayo.

Amesema, TET na TAKUKURU zimeshirikiana katika kutoa mafunzo wa watekelezaji wa Mtaala kwa walimu ili kufahamu maudhui hayo jambo litalosaidia kupata mhitimu anaejua madhara ya Rushwa.

Amesema, kupitia somo la Historia ya Tanzania na Maadili maudhui yote yanayohusu kuzuia na kupambana dhidi ya Rushwa, huku akisisitiza walimu tayari wamefundishwa njia ya kuchopeka maudhui yanayohusu Rushwa pindi wakitoa mafunzo kwa watoto.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Chalamila amesema, malengo ya ushirikiano wa TET na TAKUKURU yamefikia kwa kiasi kikubwa kwani tayari yapo maudhui ya mapambano dhidi ya Rushwa katika Mtaala ulioboreshwa amabao unatekelezwa tangu Januari 2024.

Amesema, kupitia ushirikiano huo wanafunzi ngazi ya msingi wanapata mafunzo kuhusu madhara ya Rushwa kijamii na hata kiuchumi, hivyo Kutengeneza kizazi cha wachukia Rushwa na wapenda maendeleo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...