Na Said Mwishehe, Michuzi TV


KAMPUNI ya Vodacom Tanzania,imesema katika kipindi cha miaka 25 ya kuwahudumia Watanzania inajivunia huduma mbalimbali ambazo imezianzisha ikiwemo huduma ya M-Pesa ambayo imerahisisha upatikanaji wa huduma jumuishi za kifedha nchini kote.

Katika kusherehekea miaka 25 ya Vodacom Tanzania ambayo ilianzisha huduma zake. Agosti 15 mwaka 2000 imetumia siku hiyo leo Agosti 15 ,2025 kukata keki na kusherehekea na wateja wake wakiwemo wateja wa M-Pes katika eneo la Temeke Stirio na Soko la Temeke Stirio wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa sherehe ya kukata keki ya kuadhimisha miaka 25 ya Vodacom Tanzania iliyofanyika leo katika viwanja vya Temeke Stirio , Mkurugenzi wa M-Pesa Vodacom Tanzania, Epimack Mbeteni, katika kuadhimisha siku hiyo wanajivunia mafanikio makubwa yanayokwenda sambamba na mageuzi makubwa katika huduma za kifedha.

"Kama mnavyofahamu Vodacom Tanzania tunasherehekea miaka 25 ya M-Pesa tangu tumeanza na siku kama ya leo ya Agosti 15 ndio tulizaliwa ,hivyo tumekuja mtaani kuileta M-Pesa.Tunaita M-Pesa kitaani

"Tumekuja kuzungumza na wateja wetu, tumekuja na zawadi ambazo tutawapa wateja wetu, kwahiyo tutapita mtaani tutazungumza nao tusikir wanatuambia nini kuhusiana na Vodacom na M-Pesa .Pale tunapofanya vizuri na wapi wanataka tuboreshe.

"Kwahiyo ni siku ambayo tumeitoa kwa wafanyakazi wote wa Vodacom kuja sokoni kukaa na wateja, kuzungumza, kuwasikiliza ,kutatua changamoto zao,pia kuwapa zawadi ambazo tutawapatia katika kusherehekea Birthday yetu."

Akieleza zaidi kuhusu miaka 25 ya uwepo wa Vodacom Tanzania, amesema kikubwa ambacho wanajivunia ni kuwaleta Watanzania pamoja waliokuwa hawapati kabisa huduma za kifedha kupata huduma kupitia M -pesa

"Kama mnavyofahamu wakati M-Pesa inaanza watanzania waliokuwa wanaweza kupata huduma jumuishi za kifedha ilikuwa ni kama asilimia 9 kupitia benki lakini sasa hivi huduma za kifedha kwa Watanzania ni asilimia 76 ikichangiwa na huduma kama M- Pesa ambayo imeweza kuwafikia nchi nzima,

"Pia huduma nyingi ambazo zinatatua changamoto za kawaida za Watanzania leo hii tuna huduma ya M-Koba inayowasaidia akina mama katika vikundi vyao vya VICOBA kuweka fedha zao.Kuna huduma ya mikopo kama Songesha ambazo zimerahisisha huduma za mikopo nchi nzima kupitia simu yako unaweza kupata huduma,

"Tunahuduma nyingi ambazo tumezizindua katika miaka hii yote kubwa zaidi tumeleta mapinduzi kwa maana huduma zetu ambazo tumezianzisha nabaadae wengine wameziiga lakini tunajivuni tumewafikia watanzania kwa ukubwa zaidi."

Aidha amesema huko nyuma Watanzania wanafahamu huduma za kifedha zilikuwa zinapatikana kwa kupanga foleni kama foleni ya kuchota maji, kupata mkopo wa Sh.10,000 tu ilikuwa inabidi uombe ubebembeleze lakini sasa hivi kupitia simu yako unamaliza kila kitu kwa M-Pesa.

"Ukitaka kukata bima,kuwekeza, unataka fedha, mkopo ,kulipia bidhaa,kununua bandle na chochote unachokifanya unapata kupitia M -Pesa , kwahiyo kila kitu unakipata hivyo katika miaka 25 tumefanya mapinduzi makubwa katika huduma za kifedha nchini Tanzania.'

Ameongeza katika kipindi cha miaka 25 M-Pesa imekuwa salama sana na wateja wao wanasema moja ya sababu wanaamini usalama M-pesa kwani fedha zao ziko salama na hata ikitokea changamoto wanajua watahudumiwa na hizo ndizo sababu zinazotutofautisha Vodacom na wengine."Mteja wetu anajua kuna usalama wa hali ya juu sana.".












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...