Na Mwandishi Wetu-Dodoma.

Benki ya NMB, imeanzisha huduma ya utoaji bima ya mazao na mifugo ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kusaidia kukuza sekta hizo nchini ambapo hadi sasa ng’ombe 2,000 wamekatiwa bima.

Meneja wa NMB, Kanda ya Kati Janeth Shongo, alisema hayo wakati akitoa taarifa yake kwa Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa, alipotembelea banda la benki hiyo lililopo kwenye viwanja vya maonesho ya wakulima Nane Nane jijini Dodoma.

Shongo, alisema hadi sasa ng’ombe takribani 2,000 wamekatiwa bima na wafugaji ambapo kiwango cha chini cha gharama za bima ni Sh. 20,000 na bima hizo zinathamani ya Sh. biloni 1.5.

“Kwahiyo tumeleta mapinduzi makubwa ya kuhakikisha kwamba mfugaji sasa hana wasiwasi na ufugaji wake kwa maana kwamba kama anangombe ana mbuzi na mifugo ya aina yoyote bado anaweza akakata bima na akapa usalama pale ambapo atapata majanga.

“Lakini vilevile katiba bima ya mazao tumewafikia wakulima zaidi ya 300,000 katika wakulima hao pamoja na wafugaji tumetoa bima ya takribani bilioni 659 kwa maana kwamba katika bima ya mazao tunatakribani bilioni 658 ambayo hii ina watu wengi ambao wameweza kukata bima ya mazao yao,” alisema Shongo.

Aidha, alitoa wito kwa wakulima wote ambao wanamazao yao kutumia fursa hiyo kukatiwa bima katika kilimo chao na kwenye mnyororo mzima wa thamani.

“Jambo jingine ambalo lingependa kulieleza ni katika sekta ya ufugaji tumeweza kuwakopesha wafugaji zaidi ya Sh. bilioni 100 kwa sekta ya ufugaji pekee yake. Kingine pia niwakaribishe wanchi kwa ajili ya mikopo katika mikopo tunatoa mikopo rahisi ambayo ina masharti nafuu na riba nafuu inayomwezesha mfugaji, mkulima na mvuvi kupata hahuweni kubwa sana,” alisema.

Hata hivyo, alisema katika maonesho hayo mwaka huu NMB, itaendelea kutoa elimu kwa wakulima, wafugaji pamoja na wavuvi na kuendelea kupanua wigo kwa watu wote ambao wanafanya biashara katika sekta hizo.

“Elimu tunayaoitoa tunatoa katika Vyama vya AMCOS, vikundi na katika vyama hivyo vya Ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS) tumefikia takribani AMCOS 1,139 na katika hizo AMCOS tumeweza kufikia wakulima viongozi zaidi ya 38,000 na kati ya hao 12,000 ni wanawake,” alisema.

Alisema viongozi hao wanawake watakwenda kuwafundisha wakulima wengine na mambo watakayofundisha ni pamoja na uongozi bora wa AMCOS, vikundi vyao na namna bora ya kufanya kazi katika sekta hizo za kilimo,mifugo pamoja na uvuvi.

“Ndani ya hiyo elimu tunayoitoa kwenye hii sekta ya AMCOS pia benki ya NMB tumejikita kutoa elimu vijijini katika elimu vijijini tumewezeza kufikia zaidi ya vijiji 2,000 katika vijiji ambavyo tumevifikia tumefikia zaidi ya watu milioni 2.4 ambao wamepata elimu ya fedha na kufungua akaunti na wanaweza kutumia NMB mkononi na Nmb wakala na kuendelea kunufaika na huduma za kifedha,” alisema.






 
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...