Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Michuzi TV

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, ameeleza kwamba hakuna eneo lolote nchini ambalo halijaguswa na maendeleo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Dk. Nchimbi ameeleza hayo alipohutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni za Mgombea Urais kupitia CCM Dk. Samia uliofanyika uwanja wa VETA mjini Songea jana.

“Kila Mtanzania ni shahidi kwa kasi ya maendeleo iliyofanyika nchini ikiwemo Mkoa wa Ruvuma. Umefanyakazi kubwa ya kuleta maendeleo katika maeneo yote nchi nzima. Hakuna sehemu haijaguswa na mkono wako wa maendeleo.

"Ndiyo maana leo sisi wasaidizi wako tunazunguka nchi nzima kifua mbele kunadi sera za CCM kwa sababu yapo mambo yametekelezwa chini ya uongozi wako," amesema.

Akieleza zaidi alipokuwa anawasilisha salamu za wananchi wa kabila la wasukuma ambao ni watani wa wangoni amesema wamedhamiria kuongoza kitaifa kwa kumpa Dk. Samia kura nyingi za ndiyo zikiambatana na wabunge na madiwani.

"Nimepita kwa watani wetu wasukuma wamesema wao kwa kazi alizozifanya Rais Dk. Samia wataongoza kitaifa kwa kura nyingi kwa Samia, wabunge na madiwani.

"Sasa ndugu zangu wa Ruvuma tusikubali kutaniwa na Wasukuma, tushindane na tuwashinde kwa kura nyingi. Wasukuma wamedhamiria kutushinda," amesema.

Aidha, Balozi Dk. Nchimbi alitoa msisitizo kwa Watanzania kutunza vitambulisho vyao vya kupigia kura na ifikapo Oktoba 29 mwaka huu wajitokeze kwa wingi kwenda kumpigakura Dk. Samia.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...