-Kutua mkoani Tanga Septemba 28 kwa ajili ya Kampeni kwa muda wa siku tatu.

-Wananchi watakiwa kujitokeza kwa wingi kumlaki.


Na Oscar Assenga, TANGA

MGOMBEA Urais wa Tanzania kupitia (CCM) Dkt Samia Suluhu anatarajiwa kuwasili Mkoani Tanga Septemba 28 mwaka huu na atapokelewa eneo la Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga jioni na atakuwa na ziara ya kampeni ya siku tatu .

Akizungumza leo na waandishi wa habari Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Alhaj Rajab Abdurhaman kuhusu ujio wa Mgombea huyo ambapo alisema baada ya kupokelewa atawasalimia wananchi wa eneo hilo na baadae atakwenda Tanga mjini kwa ajili ya mapumziko na siku inayofuatia ataanzia wilaya ya Pangani kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara na Tanga mjini



Akizungumzia ujio wake Mwenyekiti huyo alisema ni vizuri wananchi katika maeneo mbalimbali atakayopita mgombea huyo kujitokeza kwa wingi kumlaki kwamba anayokuja kuwahutubia ni kupitia ilani ya uchaguzi 2025/2030 baada ya kuunda Serikali maendeleo yatakayokuja kwa ajili ya wananchi wote hiyo aliwaomba wana CCM wote popote walipoo kila mmoja wanawakaribisha kujitokeza kumlaki mgombea huyo.

“Niwaombe wananchi na wana CCM wote kila mmoja tunawakaribisha kumlaki na kumpokea Mgombea wa Urais kupitia CCM hatuna mgombea mwengine zaidi ya Dkt Samia tujitokeza kwa wingi na baada ya kumalizia Mkutano Tanga mjini atapita Muheza, Korogwe na ratiba katika maeneo hayo zitatolewa kwa nyakati tofauti”Alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha alisema kwamba wana Tanga wanajiona watu wenye bahati kupata ugeni huo mkubwa kwa mara ya pili kwa mwaka huu mmoja amekuja kwa ziara ya kikazi miezi michache iliyopita mwaka huu na alikpokuja Tanga mambo mengi ya kimaendeleo ya Tanga yamefunguka na mambo yalikwenda vizuri na sasa anakuja kama Mgombea Urais.

Rajabu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu (MCC) alisema kwamba wananchi kwenye mkoa wa Tanga wanategemea maendeleo zaidi kwa sababu kuna utofauti kati ya Mgombea wa CCM na wengine kutokana na kwamba wao walihaidi na wameshafanya kupitia ilani ya uchaguzi na aliyekuwa mtekelezaji ni Rais Dkt Samia Suluhu.

Alisema kwamba kutokana na mambo makubwa ya kimaendeleo yaliyokwisha kufanyika imani yao ni kwamba wananchi watakiunga mkono chama chao kwa sababu wana imani kwamba wakihaidi wanatekeleza kwa vitendo.

Hata hivyo alisema kwamba ni wana matumaini makubwa watu watampa kura nyingi Rais Dkt Samia Suluhu kwa sababu namna alivyojipambanua katika suala la kulinda amani ya nchi kwa kutumia busara na hekima na miradi mikubwa ya maendeleo.

Alisema kwamba Dkt Samia alipokuja katika ziara ya kikazi kabla ya kuja kuna miradi ilikuwa inasuasua lakini baada ya kuja ipi miradi imefunguka mfano barabara ya Tanga-Sadani -Bagamoto kasi ilivyoongezeka na Barabara ya Soni –Bumbuli mpaka Dindira na Korogwe kupitia kwa Meta wameona barabara hiyo wataalamu wanakwenda kuanza muda msio mrefu.

Aliongeza kwamba hiyo yote ni baada ya ujio wake hivyo wanaamini anapokuja anakwenda kuwaidi yale yaliyopo kwenye ilani mpya ya uchaguzi na miradi iliyobaki itakwenda kutiliwa mkazo itamalizika na miradi mipya iweze kuanzishwa .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...