

Mgombea Udiwani wa Kata ya Maganzo, Hamza Yusuph Tandiko.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kampeni za Uchaguzi Mkuu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimeendelea kushika kasi, ambapo Mgombea Udiwani wa Kata ya Maganzo, Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Hamza Yusuph Tandiko, ameendelea kunadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030 akisisitiza kuwa ni ilani bora na mkombozi wa wananchi.
Akizungumza leo Jumapili, Septemba 28, 2025, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Sabasaba kata ya Maganzo, Tandiko amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, 2025 kupiga kura za ushindi kwa wagombea wote wa CCM kuanzia ngazi ya urais, ubunge na udiwani.

“Ilani ya Uchaguzi ya CCM ni ilani bora, imeelekeza mwanga katika sekta zote muhimu za maisha ya wananchi ikiwemo elimu, afya, miundombinu ya barabara, nishati ya umeme, maji safi na salama, uchumi na ajira, kilimo na ufugaji pamoja na michezo. Ninaomba kura kwa wagombea wote wa CCM – Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa urais, Lucy Mayenga kwa ubunge wa Jimbo la Kishapu, na mimi kijana wenu Hamza Tandiko kwa udiwani wa Maganzo,” amesema Tandiko.
Ameongeza kuwa kura za CCM ndiyo mkombozi wa Watanzania, akihimiza wananchi kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo.
Tandiko ameeleza kuwa yeye ni kijana wa kizazi kipya aliyelelewa katika maadili ya CCM na yuko tayari kuwatumikia wananchi kwa moyo wa dhati.
“Nimesimama hapa si kwa maneno tu bali kwa vitendo. Mimi ni kijana wenu, ninajua changamoto zenu na ninayo dira ya maendeleo. Kupitia Ilani ya CCM nitahakikisha maji safi, elimu bora, barabara za uhakika, ajira kwa vijana na fursa kwa wanawake na watu wenye ulemavu zinapatikana. Kura kwa CCM ni kura ya maendeleo, kura ya mshikamano na kura ya ushindi wa Maganzo,” amesema Tandiko.
Tandiko pia amezungumzia uchimbaji wa madini ya almas na kuelezea mpango wa MBT (Mining for Brighter Tomorrow) unaoendelea kutekelezwa, kama ilivyoainishwa katika Ilani ya CCM ya 2020/2025. Ameisitiza kuwa mpango huu unalenga kuongeza mapato ya taifa, kuunda ajira kwa vijana, na kuhakikisha faida za madini zinawanufaisha wananchi wote, si wachache tu.
Hata hivyo, kutokana na hali ya mvua iliyojitokeza, ameahidi kwamba atakuwa akielezea kwa kina matarajio ya CCM katika sekta ya madini katika mikutano ijayo, ili wananchi waweze kuelewa faida na fursa zilizopo.
Katika mkutano huo, viongozi mbalimbali wa CCM akiwemo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Kishapu, Jenipher Juma Nangi, wameungana na Tandiko kuomba kura kwa wagombea wa CCM, huku wakihamasisha wananchi kudumisha amani na kuwapuuza wanaotaka kuibua chokochoko za kuichafua nchi.
ANGALIA PICHA

Mgombea Udiwani wa Kata ya Maganzo, Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Hamza Yusuph Tandiko, akinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030 katika mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba Maganzo. Picha na Kadama Malunde

Mgombea Udiwani wa Kata ya Maganzo, Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Hamza Yusuph Tandiko, akinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030 katika mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba Maganzo.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Kishapu, Jenipher Juma Nangi akinadi Ilani ya CCM na kuwaombea kura wagombea wa CCM


Mkazi wa Maganzo akimpatia zawadi ya Samaki Mgombea Udiwani wa Kata ya Maganzo, Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Hamza Yusuph Tandiko baada ya kufurahishwa na sera za CCM

Mgombea Udiwani wa Kata ya Maganzo, Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Hamza Yusuph Tandiko akicheza muziki na wananchi

Mgombea Udiwani wa Kata ya Maganzo, Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Hamza Yusuph Tandiko akicheza muziki na wananchi

Mgombea Udiwani wa Kata ya Maganzo, Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Hamza Yusuph Tandiko akicheza muziki na wananchi

Mke wa Mgombea Udiwani wa Kata ya Maganzo, Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Hamza Yusuph Tandiko akiomba kura kwa wagombea wa CCM akiwemo mmewe (kulia)




















Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...