Na Mwandishi wetu, Michuzi Tv

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Rushwa na Uhujumu Uchumi, imemuhukumu Hemed Mrisho maarufu “Horohoro” kutumikia kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya cocaine zenye uzito wa gramu 326.46.

Aidha, Mahakama imeamuru dawa hizo za kulevya zilizokamatwa ziteketezwe na gari lililotumika kusafirisha dawa hizo na fedha taslimu TZS 4,100,000 zitachukuliwa kwa hatua maalum za kisheria ila baadhi ya mali binafsi za mshtakiwa arudishiwe

Akisoma hukumu hiyo Jaji Kisanya amesema ushahidi uliotolewa na mashahidi 14 wa upande wa Jamhuri na vielelezo 23, umejitosheleza na umeweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka yoyote kuwa Hororo alitenda kosa hill.

Horohoro alikamatwa Oktoba 31, 2023 katika eneo la Boko Magengeni, Kinondoni – Dar es Salaam, akiwa anaendesha gari aina ya BMW X5 lenye namba za usajili T189 DWY.

Ndani ya gari hilo, maafisa wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya (DCEA) walipata mfuko mwekundu wenye unga uliothibitishwa na Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) kuwa ni cocaine yenye uzito wa gramu 326.46.

Katika kesi hiyo pande wa mashtaka uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Gloria Kilawe, Marietha Maguta na Hamis Katandula ambao waliweza kuthibitisha kuwa mshtakiwa alikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na dawa hizo haramu.

Upande wa utetezi, ukiongozwa na Mawakili Augustine Kusalika na Nehemia Nkoko,ulijaribu kupinga ushahidi kwa kudai kuwa mshtakiwa alikamatwa kabla ya tukio na kwamba kesi ilichochewa na chuki binafsi. Hata hivyo, hoja hizo zilitupiliwa mbali na Mahakama, ikiridhia ushahidi wa Jamhuri.

Kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Sura ya 95 (R.E. 2023), kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito unaozidi gramu 200 adhabu yake ni kifungo cha maisha jela.Hivyo, hukumu hii ni onyo kali kwa jamii kwamba biashara ya dawa za kulevya haitavumiliwa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...