Na Said Mwishehe,Michuzi TV -Ruangwa
MWANAMUZIKI maarufu katika muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Fleva Rajabu Ibrahim maarufu Harmonize leo amewapagawisha wana CCM na wananchi wa Ruangwa mkoani Lindi baada ya kuimba Wimbo wa Namleta Rais ambao ni wa Msanii Nassib Abdull ‘Diamond’
Kwa muda mrefu Harmonize tangu alivyoondoka Lebo ya WCB ya Wasaf inayomilikiwa na Diamond amekuwa akifanya muziki wake kupitia lebo yake ya Conde Gang lakini leo ameonesha namna ambavyo anaweza kuuimba Wimbo wa Namleta Rais ambao umeimbwa na Diamond.
Wimbo huo ni moja kati ya nyimbo ambazo zimetokea kupendwa na wanachama,mashabiki na wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi na leo Hamornize ameuimba huo mbele ya mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Mbunge wa Ruangwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Ustadi wa Hamornize wakati akiimba Wimbo huo akisindikizwa na wanamuziki wa bendi ya TOT ulimfanya Dk.Samia kushindwa kujizuia hivyo aliamua kusimama na kuanza kucheza .
Kwa waliokuwa wanafuatilia Hamornize akiimba Wimbo huo kuna wokati ilikuwa ni ngumu kısmını kama anayeimba ni Harmonize au Diamond maana alitumia sauti na vionjo bilebile ambavyo Diamond amekuwa akivutumia anapoimba wimbo huo.
Kwa kifupi Kampeni za mgombea urais CCM Dk.Samia Suluhu Hassan kwa siku ya leo ni kama zimemrudisha Harmonize katika familia ya Diamond kwani huko zamanı wakiwa pamoja walishirikiana kuimba pamoja kwa baadhi ya nyimbo. Pamoja na burudani hiyo ya Hamornize usisahau kuwa Oktoba 29 mwaka huu tiki yako ya mgombea urais unakiwa kuiweka kwa Dk.Samia Suluhu Hassan.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...