Akizungumza jana jioni kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), kwa ajili ya kuwasilisha pongezi maalum kwa mwanariadha huyo, Simbu alisema licha ya ushindani mkubwa aliupata kutoka kwa wanariadha wa kimataifa kwenye mashindano hayo ya Tokyo bado aliweza kuhimili ushindani kutokana na maandalizi pamoja na morali kubwa aliyokuwa nayo kufutia ushindi wa awali aliokuwa ameupata kwenye mbio za km 21 za NBC Dodoma Marathon zilizofanyika mwishoni mwa mwezi Julai jijini Dodoma.
Hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya benki ya NBC jijini Dar es Salaam ilihusisha maofisa waandamizi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Theobald Sabi, pamoja na wadau wa mchezo wa riadha wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bw Rogath John Akhwari alieambatana na baadhi ya wanaridha akiwemo Simbu.
“Ushiriki na ushindi wangu kwenye mbio za KM 21 za NBC Dodoma Marathon mwezi Julai ilikuwa kama chanzo cha morali niliyokuwa nayo niliposhiriki kwenye mashindano ya kimataifa ya Riadha ya Tokyo. Nilitumia mbio za NBC Dodoma Marathon kama kipimo cha kujua utimamu wangu kimwili na ushindi wangu pale Dodoma ndio ulikuwa mwanzo wa ushindi wangu jijini Tokyo.’’
“Nawashukuru sana waandaaji wa mbio za NBC Dodoma Marathon, Benki ya NBC kwa kuandaa mbio zenye ushindani ambazo kwasasa tunazitumia kama kipimo sahihi cha utimamu wetu kabla ya kushiriki mashindani makubwa zaidi ya kudunia,’’ alisema Simbu.
Zaidi Simbu aliwashukuru wadau mbalimbali nchini ikiwemo Serikali na benki hiyo kwa kwa pongezi nyingi kufuatia ushindi wake huku akiwapongeza wadau hao kwa jitahada zao katika kukuza mchezo wa riadha hapa nchini.
“Nimepokea salamu za pongezi nyingi ikiwemo kutoka kwa viongozi waandamizi kabisa wa serikali akiwemo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, nashukuru sana kwa hilo na leo hii nipo hapa kupokea pongezi rasmi kutoka benki ya NBC ambao kiukweli wamekuwa ni wadau muhimu sana kwenye sekta ya michezo ukiwemo mchezo wa riadha. Hatua ya NBC kuandaa tukio hili la pongezi kwangu ni uthibitisho tosha za utambuzi wao kwa mchezo huu riadha…nawashukuru sana’’ alisema Simbu.
Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, Sabi alielekeza pongezi hizo kwa RT pamoja na wadau wengine wa mchezo huo ikiwemo serikali kufuatia mafanikio makubwa yanayoendelea kushuhudiwa kwenye mchezo wa riadha hususani hivi karibuni.
“Kwa niaba ya Bodi na Menejimenti ya Benki ya NBC , natoa shukrani za dhati na maalum kwa uongozi wa riadha Tanzania pamoja na Alphonce Simbu kwa kutuwakilisha vyema katika riadha za kimataifa na kupeperusha bendera ya Tanzania duniani kwa ushindi. Akiwa kama mwanafamilia kinara wa mbio za NBC Dodoma Marathon, Simbu alitumia muda wa 2:09:48 kwenye mbio hizo za Tokyo na hivyo kuandika sehemu ya historia ya taifa letu…pongezi nyingi sana kwake,’’ alisema Sabi.
Kwa upande wake Rais wa RT, Akhwari aliwasilisha shukrani za wadau mbalimbali wa mchezo huo kwa benki ya NBC kufutia mchango wake mkubwa kwenye mchezo huo huku akiitaja mbio ya NBC Dodoma Marathon kama kipimo sahihi kinachotumiwa na wanaridha wa Kitanzania kwasasa kabla ya kushiriki kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa.
“Medali hii aliyoileta Simbu haijawahi kuletwa nchini hapo kabla. Ila imekuja kipindi hiki ambacho NBC Dodoma Marathon imekuwa mbio yenye hadhi zaidi ya kimataifa. Hatua hii ni uthibitisho tosha kuwa kwasasa hapa nchini tuna mbio ambazo tunaweza kuzitumia kama kipimo sahihi kujipima kimataifa na zikatupa majibu sahihi. Hapa tunapozungumza kuna washindi wengine walioshika nafasi ya pili kwenye mbio hizi hizi mwezi Julai nao leo (Jumatano) wamefanya vizuri sana kwenye mbio nyingine huko Afrika Kusini’’ alisema Akhwari.
Alisema kwasasa shirikisho hilo lipo kwenye mchakato wa kutekeleza program ya kisasa ya kuandaa vijana na watoto kwenye mchezo huo ili kuandaa kizazi kijacho kitakachoendeleza mafanikio yanayoendelea kushuhudiwa kupitia mchezo huo.
Mwanaridha wa kimataifa wa Tanzania na mshindi wa mbio ndefu za Mashindano ya Kimataifa ya Riadha ya Tokyo Alphonce Simbu (katikati) akimuonesha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kushoto) muonekano wa medali ya dhahabu aliyoipata kupitia mashindano hayo wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya kumpongeza mwanariadha huyo hiyo jijini Dar es Salaam jana jioni. Kulia ni Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bw Rogath John Akhwari.
Mwanaridha wa kimataifa wa Tanzania na mshindi wa mbio ndefu za Mashindano ya Kimataifa ya Riadha ya Tokyo Alphonce Simbu (kushoto) na Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bw Rogath John Akhwari (kulia) wakimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (katikati) zawadi ya jezi maalum ya timu ya Taifa ya Riadha iliyosainiwa na mwanaridha huyo ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa benki hiyo katika kuendeleza mchezo wa riadha nchini hususani kupitia mbio zinazoandaliwa na benki hiyo za NBC Dodoma Marathon. Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya kumpongeza mwanariadha huyo hiyo jijini Dar es Salaam jana jioni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kushoto) akimshuhudia Mwanaridha wa kimataifa wa Tanzania na mshindi wa mbio ndefu za Mashindano ya Kimataifa ya Riadha ya Tokyo Alphonce Simbu (kulia) akisaini jezi maalum ya timu ya Taifa ya Riadha kabla ya kuikabidhi kwa mkurugenzi huyo kama zawadi ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa benki hiyo katika kuendeleza mchezo wa riadha nchini hususani kupitia mbio zinazoandaliwa na benki hiyo za NBC Dodoma Marathon. Tukio hilo lilifanyika wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya kumpongeza mwanariadha huyo jijini Dar es Salaam jana jioni.
Hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam ilihusisha maofisa waandamizi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bw Theobald Sabi (wa tatu kushoto) pamoja na wadau wa mchezo wa riadha wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bw Rogath John Akhwari (wanne kulia) alieambatana na baadhi ya wanaridha akiwemo Simbu (Katikati). Kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko wa benki ya NBC, David Raymond
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kulia) akimshuhudia Mwanaridha wa kimataifa wa Tanzania na mshindi wa mbio ndefu za Mashindano ya Kimataifa ya Riadha ya Tokyo Alphonce Simbu (kulia) akisaini kitabu cha wageni wakati mwanariadha huyo pamoja na wadau mbalimbali wa mchezo wa riadha nchini akiwemo Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bw Rogath John Akhwari walipofika makao makuu ya benki ya NBC jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki hafla fupi iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya kumpongeza mwanariadha huyo jijini Dar es Salaam jana jioni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kushoto) akimpongeza Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bw Rogath John Akhwari kwa mafanikio mbalimbali ya mchezo wa riadha nchini ikiwemo ushindi wa Mwanaridha wa kimataifa wa Tanzania na mshindi wa mbio ndefu za Mashindano ya Kimataifa ya Riadha ya Tokyo Alphonce Simbu wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya kumpongeza mwanaridha huyo kufuatia mafanikio hayo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana jioni.
Mwanaridha wa kimataifa wa Tanzania na mshindi wa mbio ndefu za Mashindano ya Kimataifa ya Riadha ya Tokyo Alphonce Simbu (kushoto) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kulia) wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya kumpongeza mwanaridha huyo kufuatia mafanikio hayo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana jioni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya kumpongeza Mwanaridha wa kimataifa wa Tanzania na mshindi wa mbio ndefu za Mashindano ya Kimataifa ya Riadha ya Tokyo Alphonce Simbu (kushoto).Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana jioni. Kulia ni Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bw Rogath John Akhwari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...