Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile, amelipongeza shirika la umeme Tanzania TANESCO kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwani amekuwa akipokea zawadi kutoka kwa wateja wa shirika hilo waishio maeneo ya vijijini kumpongeza kwa jitihada zinazofanywa na TANESCO kufikisha huduma kwenye vijiji vyote.
Mbali na mafanikio hayo, amewataka TANESCO kufanya uhakiki na ufuatiliaji kwa wakandarasi ili kujiridhisha na watumishi wanaowaajiri kwenye maeneo ya miradhi kama ni waaminifu, akitolea mfano wa malalamiko aliyowahi kuyapokea kutoka kwa wananchi wakilaghaiwa kutoa pesa n.k.
Amesema baada ya malalamiko hayo timu ya TANESCO makao makuu ilifika kuchunguza na kubaini tatizo baadae kutatua. Amewapongeza kwa kuendelea kuwa taasisi ya mfano inayoshughulikia changamoto kwa vitendo.
TANESCO Mkoani Ruvuma ilimkabidhi zawadi na pressure cooker ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ya umeme ikiwa ni mwendelezo wa wiki ya huduma kwa wateja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...