-Awataka watanzania kutoka kwa wingi kupiga kura kumchagua Dkt Samia Suluhu,Wabunge na Madiwani wanaotokana na CCM.

Na Oscar Assenga,MUHEZA.

MKURUGENZI Mstaafu wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Balozi Adadi Rajabu amesema kwamba suala la amani na utulivu ni muhimu Octoba 29 mwaka huu kupiga kura huku akiwataka watanzania kujitokeza kwa wingi na kwamba siku hiyo hakutakuwa na maandamano yoyote kutokana na uimara wa vyombo vya ulinzi hapa nchini.
 

Balozi Adadi aliyasema hayo wakati wa mkutano wa kampeni wa kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwinjuma alimaarufu Mwana FA katika halfa ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhamani ambapo alisema suala la amani ni muhimu sana

Alisema kwamba anasema hayo kutokana na kwamba yeye amekulia kwenye vyombo na anajua vyombo hivyo vinafanya nini vipo kwenye mazoezi kuangalia wale ambao wataleta chokochoko Octoba 29 washughulike nao.

“La mwisho suala la amani na utulivu Octoba 29 ni muhumu kuna watu wametokea wanaleta chochoko kwenye mitandano kwamba kuchafua na maandamano nawahakikishia hakutakuwa na maandamabo vyombo vipo imara”Alisema

“Niwaambie kwamba mimi nimekulia kwenye vyombo na najua vyombo vinafanya nini vipo kwenye mazoezi kuangalia wale ambao wataleta chokochoko Octoba 29 nawaomba mtokea kwa amani ikiwemo misusuru ya kwenda kwenye vituo vya kupigia kura mimi nitapiga kura Kerenge”Alisema

Aidha alisema kwamba baada ya kupiga kura ataangalia hali ya usalama inaende vipi hivyo kuwataka watoke wasiwe na hofu yoyote kwamba kutakuwa na watu gani ambao watawashauri waangamane wewe umeshaona watu wa aina hiyo.

“Vitu vya namna hii havijawahi kutokea sijaona mimi kulikuwa na ndugu zangu Waislamu miaka nipo kazini kulitokea maandamano mengi kule Magomeni kwa hiyo wachache wakafungwa ,wachache wakaenda jela”Alisema

Alisema kwamba lakini wale walivyotoka jela wakasema yale yalikuwa ni mambo ya kipumbavu wenzao waliwauza kuna wenzao waliwauza wao hawakutokea walikaa nyuma nyuma wao walikuwa mbele wakadakwa wakafungwa na kueleza hawarudiii tena hilo ni somo hivyo wapige kura kwa amani na utulivu bila matatizo yotote .

Balozi Adadi aliwambia wana Muheza katika mkutano huo kwamba wana kila sababu ya kumchagua Dkt Samia Suluhu kwa sababu ya mambo ambayo ameyafanya katika kipindi cha miaka minne kipovu haambiwa tazama ukiangalia malengo kila upande samia amegusa na uchumi umeongezekana na upo juu ukiangalia sekta ya miundombu barabara za lami nchi nzima.

Alisema pia ukiangalia ndege ambazo zimekuja zipo zaidi ya 15 pamoja na treli ya SGR watu siku hizi wanalala Dodoma wanakwenda kufanya kazi Dar huku wanalala Morogoro wanakwenda kufanya kazi Dar yote ni uchumi kuongezeka kwa kasi,.

Akizungumzia watalii alisema kwamba yeye alikuwa Balozi nchini Zimbabwe kivutio cha utalii ni kimoja tu Victoria Falls wale walikuwa wanaingiza watalii 2,500 na Samia Suluhu alivyoingia madarakani hapa nchini kuna vivutio vingi sana pamoja na vyote hivyo lakini watalii ambao walikuwa wanaingia walikuwa hawafiki Milioni 1 sasa hivi baada ya Royal Tour na sio raisi kufanya hivyo.

Alisema lakini Dkt Samia Suluhu alivunja rekodi aliingia na kufanya filamu ya hiyo na sasa wanaingiza watalii Milioni 5 na nusu lakini pia amefanya mambo mengi sana na uchumi umepanda kwa kiasi kikubwa sana na hata mfumuko wa bei upo katikati ni kitu cha kujivunia.

Hata hivyo aliwaomba wananchi wa Jimbo la Muheza kumchagua Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo (CCM) Hamisi Mwijuma alimaarufu Mwana FA kwa sababu ni Mbunge k mwenye uwezo wa kila kitu na hatuwezi kuwa na mbunge anakuwa njaa badala ya yeye kuombwa yeye anaomba.

“Jamani Muheza tunahitaji Mbunge kama huyo ?hatuwezi kuwa na mbunge ambaye anaambiwa zahanati haijapauliwa anagonjea fedha ya Serikali sasa si kichekesho hicho,”Alisema

Balozi Adadi alisema kwamba anamuona mwana FA ndio mbunge ambaye anaweza kuongoza wilaya ya Muheza kutokana na uwezo wake akiingia bungeni sio bubu wala kukaa mjengoni kwani kuna wabunge wana lala miaka 5 hawajafungua mdomo.

“Mimi sikugombea safari hii na sidhani kama nitagombea tena lakini nilimuita mwana FA tukaongea yeye ndio anastahili kushika Jimbo la Muheza yeye ndio mwenye uwezo yeye akiingia bungeni sio bubu wala kukaa mjengoni kuna wabunge wengine wana lala miaka 5 hajafungua mdomo kuzungumza”Alisema

Aliwataka wana Muheza wamuombee ili aweze kuingia tena mjengoni aweze kuchaguliwa kuwa Waziri hiyo ni sifa ya Muheza unapokuwa waziri unakuwa na Faida na una uwezo wa kuongea na Mawaziri wenzake ,makatabu wakuu wowote ili Muheza iweze kupata msaada.

Hata hivyo alisema kwamba hata mbunge anatakiwa awe na nguvu ya kugonga kokote na hawahitaji wabunge waoga waoga hivyo lakini pia chagueni na madiwani ambao ni mahiri ambao wanaendea kutuletea maendeleo.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...