Na Said Mwishehe,Michuzi TV.
MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema Serikali katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imefanya kazi nzuri ya kujenga barabara za Mabasi yaendayo haraka(BRT).
Akihutubia maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Oktoba 22,2025 wakati wa mkutano wa kampeni Dk.Samia amesema kwa Ilala wamefanya kazi nzuri ya kujenga barabara zq BRT.
“Ujenzi wa barabara za zile Ilala inapendeza nikitoka Ikulu kwenda Uwanja wa Ndege(Airport mpaka nasikia raha njia iliyokuwa pana ,ilivyofunguka usafiri unavyokwenda.
“Kuna siku nilikasirishwa sana na nilifokea baraza langu la mawaziri nilitoka safari usiku natoka Airport nakwenda Ikulu nakuta makundi ya watu wanasubiri usafiri mabasi hakuna ,lile wana Ilala na wana Dar es Salaam sasa hakuna.
“Tuna kampuni nne zitakazoweka mabasi njiani, kila njia inapomalizika na nilishazitaja nilipokuwa Kinondoni jana, ndugu zangu Ilala usafiri tunakwenda vizuri lakini ujenzi barabara za ndani ya Wilaya ndani ya majimbo yako vizuri.
Kuhusu huduma za afya amesema Serikali imefanya kazi katika sekta ya afya na kwasasa huduma za afya zinapatikana kwa karibu zaidi ukilinganisha na zamani
“Katika miaka mitano au sita iliyopita Tanzania hapa hatukuwa tunafanya operesheni za matundu ya moyo leo tunafanya,
hatukuwa tunapandikiza uoto kwenye uti wa mgongo leo tunapandikiza.Tanzania leo tunapandikiza figo.
“Tanzania leo tunafanya operesheni kubwa ambazo zamani wagonjwa wetu tuliwapeleka nje sasa tunafanya ndani ku Save-pesa zetu za kigeni tuzihifadhi zitumike kufanya mambo mengine.Kwahiyo hatujamaliza tunaendelea lakini makubwa yamefanyika.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...