Na Said Nwishehe,Michuzi TV-Manyara

MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amehutubia maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara huku akitumia nafasi hiyo kueleza kuwa tayari Serikali imetoa fedha kununua mitambo ya kuondoa magugu kwenye maziwa yote nchini likiwemo Ziwa Babati.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni kuelekea Oktoba 29 ,2025 mbele ya wananchi wa Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara Dk.Samia amesema kuhusu magugu maji katika ziwa Babati pamoja na maziwa mengine nchini Serikali imetoa fedha kununua mitambo ya kuondoa magugu kwenye maziwa yote nchini.

“Serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya kununua mitambo ya kusafisha magugu maji katika maziwa na sio tu katika ziwa Babati bali katika maziwa yote nchini kutakuwa na mitambo ambayo itatumika kuondoa magugu maji.”

Dk.Samia amesema katika Ilani ya uchaguzi kifungu cha 26 (1) inasema Serikali itatekeleza mpango wa matumizi maeneo ya bahari na maji baridi kwa kushirikiana na wananchi lengo kuleta manufaa.

Hivyo, amesema moja ya kazi hiyo ni kuondoa magugu katika maziwa mbalimbali nchini."Serikali imejipanga vyema na ilani imetuelekeza kuyafanyiakazi maeneo hayo," amesema DK.Samia ambaye alitoa maelezo hayo kufuatia ombi la wananchi kuomba magugu maji katika ziwa hilo yaondolewe.

Kuhusu ombi la vizimba vya ufugaji samaki, Dk.Samia amesema ombi hilo litakwenda kufanyiwa kazi chini ya programu ya Jenga Iliyokesho Bora (BBT).

Wakati huo huo akizungumzia maeneo ambayo wawekezaji walihodhi leseni za uchambaji madini kwa muda mrefu bila kuyaendeleza amesema Serikali imefuta leseni.

Amesema maeneo hayo yamegawiwa kwa wachimbaji wadogo ambao baada ya kupima kisha kubaini maeneo mengine kipaumbele kitakuwa kwa wachimbaji wadogo.

Pia, amesema kuwa mkoa huo umenufaika kupitia ujenzi wa vihenge vikubwa vya kuhifadhia mazao lengo kuongeza kiwango cha kuhifadhi mazao.

“Serikali imejenga bwawa na skimu ya umwagiliaji Mbulu ambayo imeshakamilika na kuwanufaisha wananchi zaidi ya 2,400.”

Kuhusu uimarishaji mawasiliano ya simu, amesema upatikanaji wa mawasiliano umeongezeka kutoka asilimia 83 hadi 93 huku akifafanua hatua hiyo ni matokeo ya ujenzi wa minara 17 ya simu eneo la Simanjiro, 21 Kiteto na mitano wilayani Hanang.

Katika hatua nyingine akiizungumzia sekta ya kilimo na mafanikio yaliyopatikana Dk. Samia amesema Serikali ina kanzidata ya wakulima nchini ambapo mkulima itamwezesha kupata mbegu na mbolea ya ruzuku.

"Kwa maana hiyo lazima tuhakikishe mawasiliano yanapatikana kote vijijini, hayo ndiyo tunapoelekea," amesema mgombea urais Dk.Samia.

Wakati huo huo amesena CCM inaamini kuwa kielelezo bora cha maisha ya watu ni upatikanaji huduma bora za jamii kwa wote.

Ameongeza ndio maana wakati Hanang ilipokumbwa na janga la maporomoko ya udongo serikali ilijenga makazi ya gharama nafuu kwa wananchi."Serikali ya CCM tumejipanga vyema na tumerudi kwenu kuomba ridhaa kuongoza nchi.”

Dk.Samia amesema katika miaka mitano ijayo serikali itaongeza kasi ya uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda katika wilaya za mkoa huo na hatua hiyo itawezesha kuongeza thamani ya mazao yanayolimwa katika maeneo mbalimbali.

Kuhusu uchaguzi mkuu amesema umefanyika kwa fedha za ndani bila kusaidiwa kutoka nje ya nchi hatua ambayo Tanzania inajivunia hivyo akatumia nafasi hiyo kueleza licha ya kutumia fedha kufanya uchaguzi anaamini baada ya uchaguzi mambo yatakuwa sawa na miradi ya maendeleo itatekelezwa kwa kasi zaidi lengo likiwa kulinda utu wa mtanzania.





Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...