Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Mkuranga

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ameahidi kuondoa msongamano uliopo Kongowe hadi Mkuranga mkoani Pwani kwa kujenga barabara ya njia nne.

Kwa mujibu wa Mgombea Urais Dk.Samia ni kwamba msongamano katika eneo hilo unachangia ucheleweshaji wa usafiri na kuathiri shughuli za uchumi.

Akizungumza leo Oktoba 20,2025 mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkuranga mkoani Pwani ambapo anaendelea na mikutano ya kampeni, Dk.Samia amesema iwapo Chama chake kitapata ridhaa ya kuongoza nchi itakwenda kumaliza msongamano huo kwa kujenga barabara ya njia nne kutoka Kongowe hadi Mkuranga.

“Waziri wa Ujenzi ni kijana ninayemuamini na anatoka hapa Mkuranga hivyo ataangalia aone nini kinaweza kufanya.”

Kuhusu barabara ya Mkuranga mjini hadi Kisiju nayo iko katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2025-2030 na itakwenda kufanyiwa kazi na ikikamilika itasaidia pia bandari ya Kisiju kwani barabara hiyo inakwenda huko.

Kwa upande wa ombi la ujenzi wa Kituo cha mabasi ya kwenda mikoa ya Kusini kijenge eneo la Mkuranga Dk.Samia amesema ujenzi wa kituo hicho uko katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu hivyo katika miaka mitano ijayo inakwenda kujengwa.

“Ujenzi wa kituo cha mabasi ya Kusini iko katika Ilani hivyo itakwenda kujengwa na Mkuranga iko tayari kwa ajili ya kujengwa kwa kituo hicho na ndio maana imeandaa kwa kutenga eneo la kujengwa kituo hicho.

“Serikali tuko tayari kujenga kituo cha mabasi ya kusini lakini tunataka eneo ambalo halitahitaji kulipia fidia na Mkuranga wameshatenga eneo na tunaamini halitahigaji fidia.”

Kuhusu maji mgombea Urais Dk.Samia ameahidi yatafika Panzuo,Mkamba na Kisegese huku akieleza pia kuna awamu ya pili ya mradi wa ambayo itapeleka maji maeneo ambayo maji hajafika katika Wilaya ya Mkuranga.

Wakati huo huo amesema kwamba Serikali ya Awamu ya Sita ni ya watu na inafanya kazi ya watu kwa ajili ya kustawisha maisha ya watu ndio maana wanaseka Kazi na Utu huku akifafanua kuwa yote yanayofanywa katika kuleta kuboresha huduma za jamii ni kunalenga utu wa mtu.

Hivyo amewaomba wananchi Oktoba 29 mwaka huu wajitokeze kwa wingi wakachague Chama Cha Mapinduzi(CCM).

“Kachagueni Chama Cha Mapinduzi kwa wingi huu wa mkutano ndio ukatafsirike katika sanduku la kura, twendeni tukapige kura msinuvunje nguvu nikashindwa kufanya tuliyopanga Mkuranga.”




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...