Songea_Ruvuma.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, amewataka Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na walimu wa Mkoa wa Ruvuma kutumia nafasi yao ya kukubalika katika jamii kuhamasisha wananchi waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura katika uchaguzi tarehe 29 mwezi huu.

Dkt. Ndumbaro amesema hayo wakati akifungua mafunzo maalum kwa viongozi wa kitengo cha walimu wanawake Mkoa wa Ruvuma yaliyoandaliwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Ruvuma, kwa ajili ya kuwawezesha viongozi hao kwenda kusimamia vyema majukumu yao sehemu za kazi na kuwapa elimu ya kukabiliana na vitendo mtambuka ikiwemo ukatili wa kijinsia.

Aidha, Dkt. Ndumbaro ambaye pia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Songea Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi, amewaomba walimu kuendelea kukiunga mkono Chama hicho kwa kumpigia kura Mgombea Urais Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa CCM.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mwenye huruma anayejali maslahi ya watu wakiwemo walimu, na kwamba katika kipindi kifupi cha miaka minne amefanikisha kupandisha madaraja ya walimu, kuajiri walimu wapya na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kujenga madarasa, ofisi za walimu na maabara.

Dkt. Ndumbaro aliwahakikishia walimu kuwa changamoto zinazowakabili, ikiwemo madai ya fedha za uhamisho na kupandishwa madaraja kwa wakati, tayari zimeanza kushughulikiwa na Serikali ya awamu ya sita.

Alisema kwa wale waliobahatika kufanya kazi kwa karibu na Dkt. Samia Suluhu Hassan wanatambua kuwa kauli yake ya “Kazi na Utu” haiko mdomoni bali inatoka moyoni, na kwamba tangu aingie madarakani ameongeza mishahara, ajira mpya na kulipa madeni mbalimbali.

Alieleza kuwa walimu, hasa wanawake, wana nafasi kubwa ya ushawishi katika jamii, jambo linalofanya hata wanaume wengi kuvuti.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...