*Ni maelfu kwa maelfu ya wananchi wakimfuatilia na kumsikiliza Dk.Samia
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Shinyanga
HAKIKA wananchi wa Kahama leo wameonesha ‘True love’ kwa mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),Dk.Samia Suluhu Hassan katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Magufuli mjini Kahama ambapo maelfu ya wananchi walifurika.
Umati uliofika katika Uwanja huo kwa jicho la kawaida umevunja rekodi kutokana na idadi kubwa ya watu waliohudhuria kwani sio maelfu ya watu bali ni utitiri wa watu.
Uwanjani watu walikuwa wamejaa hakuna pakukanyaga lakini wakati unafikiria marufuriko ya walioukuwa uwanjani nje ya Uwanja nako kulikuwa na maelfu ya watu ambao walikuwa wakifuatilia mkutano wa kampeni za mgombea Urais Dk.Samia.
Shangwa za maelfu ya wananchi ambao muda wote walikuwa na Vibe ilikuwa aina nyingine ya burudani kwani licha ya watu yao kumsubiria mgombea Urais Dk.Samia kuanzia mapema kabisa lakini hakuna aliyekuwa amechoka.
Kahama wameonesha true Love kwa Dk.Samia Suluhu Hassan na ukweli wameshaamua Oktoba 29 wana Tiki kwa Samia.Ni kweli Dk.Samia katika mikutano yake maelfu ya wananchi wamekuwa wakihudhuria na huenda ikawa ngumu kupima kwa macho lakini kwa Kahama wanaingia katıka rekodi yao.
Hata hivyo nyota njema huonekana asubuhi kwani Mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan akiwa katika Uwanja wa Kambarage uliopo Shinyanga Mjini nako kulifurika maelfu ya watu.Umati mkubwa wa watu ulimfanya mgombea Urais Dk.Samia kutoa Saluti kwa wananchi wa Shinyanga.
Lakini Kahama kumbe walikuwa na jambo lao ,kwa lugha rahisi wananchi wa Kahama umati wa watu ni kama vile Nje Ntiti ndani Ntiti.Walio uwanjani kama waliko nje na walioko nje ni kama walioko uwanjani.
Katika barabara za Kahama Mjini ambako mgombea Urais Dk.Samia alikuwa anapita na Msafara wake maelfu ya wananchi walikuwa wamejipanga barabarani wengine wakawa na simu zao wakirekodi msafara na wengine wakipiga ‘Selfie’ na Mama.Hakuna aliyetaka kujipunja.
Kwa siku ya leo hapa Kahama ni kama ilikuwa sherehe ya kitaifa,jinsi ambavyo maelefu ya watanzania wamejitokeza kumsikiliza Chiefu Hangaya akimwaga sera.
Halafu ni hivi alipowasili uwanjani sasa umati ulilipuka kwa kelele na vigelegele Mwenye kuimba twende Mwenye kucheza twende ilimradi ni burudani kwa kwenda mbele.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...