DUBAI, UAE
Benki ya NMB imepokea tuzo maalum ya kuwa benki ya kwanza katika Afrika Mashariki kutoa kadi maalum iliyobuniwa kwaajili ya wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs).
Tuzo hiyo ilikabidhiwa jijini Dubai kwa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Bw. Filbert Mponzi, na Makamu wa Rais, Malipo ya Mastercard, Bi. Prakrithi Singh, katika hafla ya kitaifa.
Hafla hiyo ya utoaji tuzo ilihudhuriwa pia na viongozi wengine wa NMB, ikiwemo Mkuu wa Idara ya Biashara, Bw. Alex Mgeni, na Meneja Mwandamizi kutoka Idara ya Kadi, Bw. Manfred Kayala.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...