Na MWANDISHI WETU.

TAASISI ya Saratani Ocean Road kwa kushirikiana na Benki ya Exim, wameendesha kambi maalumu ya uchunguzi wa saratani kwa wafanyakazi, wateja pamoja na wananchi ili kujua afya zao hususan ugonjwa wa saratani.

Akizungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu ya benki hiyo, Meneja wa Huduma za Saratani wa taasisi hiyo, Dar es Salaam, jana, Dk. Maguhwa Stephano, alisema lengo la kambi hiyo ni kutoa elimu na uchunguzi wa saratani, kwa sababau saratani ukigundulika mapema inatibika.

Maguhwa alisema mwezi oktoba ni mahususi duniani wa kuhamasisha uelewa wa saratani ya matiti, hivyo wameweka kipaumbele kwa kuelimuisha na kufanya uchunguzi wa mbalimbali katika Taasisi ya Saratani Ocean Road.

"Leo tumeungana na benki ya Exim hapa makao makuu katika wiki kuadhimisha wiki ya huduma kwa mteja, pia hii wiki ya kuhamasisha suala la saratani ya matiti, kwa hiyo timu yetu iko hapa tunatoa elimu na uchunguzi wa  saratani hususan saratani ya matiti", alisema.

Aidha Maguhwa amewata wananchi na wateja wa benki hiyo kujitokeza kufanyiwa uchunguzi wa saratani mbalimbali ili kujua afya zao bila malipo.

Alisema saratani ikigundulika mapema inatibika, hivyo haiwezi kugundulika bila kufanyiwa uchunguzi, wananchi wafanye uchunguzi wa mara kwa mara.

Kwa upande wa Meneja wa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Kauthar D'Souza, alisema wameweka kambi hiyo kwa kengo la kuadhimisha mwezi wa Oktoba wa uelewa kuhusu saratani pamoja maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja, hivyo wametoa fursa hiyo kwa wateja na wafanyakazi kufanya uchunguzi wa afya zao, hususan saratani ya matiti.

Alisema watu wakifahamu afya zao hususan suala la saratani itakuwa rahisi kupata matibabu na kuwakaribisha wateja wa benki hiyo pamoja na wananchi wengine kufanya uchunguzi wa afya zao.

Naye Shujaa wa Saratani Cedou Said Mandingo, ameipongeza taasisi ya Saratani Ocean Road na benki hiyo, kwa kuandaa kambi hizi muhimu, ambazo huleta matokeo chanya kwasababu saratani ikigundulika mapema inatibika.

"Watu wengi wanaoukutwa na saratani katika hatua za awali matibabu yao huwa mepesi na kupona inakuwa uhakika zaidi, lakini ukichelewa na kufika hatua za mwisho hata matibabu huwa ya gharama kubwa, hivyo wafanyakazi, wateja na wananchi wajitokeze kufanyiwa uchunguzi", alisema.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...