Sanlam na Allianz, makampuni mashuhuri katika sekta ya bima ambao waliungana pamoja mwaka 2023 kuunda kampuni kubwa zaidi barani Afrika ya huduma za kifedha zisizo za benki, SanlamAllianz, wamezindua rasmi chapa ya SanlamAllianz nchini Tanzania leo.
Uzinduzi umefanyika katika Hoteli ya Johari Rotana, Dar es Salaam.Uanzishwaji wa SanlamAllianz General Insurance Tanzania Ltd na SanlamAllianz Life Insurance Tanzania Ltd unaonyesha utekelezaji endelevu wa uanzishaji wa chapa hii mpya katika nchi mbalimbali barani Afrika.
Viongozi wakuu wa makampuni haya ni Jaideep Goel, Mkurugenzi Mtendaji wa SanlamAllianz General Insurance, na Julius Magabe, Mkurugenzi Mtendaji wa SanlamAllianz Life Insurance.
SanlamAllianz inalenga kutumia utaalamu wake wa kimataifa wa pan-Afrika kufungua fursa za ukuaji katika uchumi wenye uwezo mkubwa barani Afrika.
Ikiongozwa na lengo lake la kuwezesha vizazi kujiamini kifedha, kuwa na usalama na kustawi, kampuni hii inataka kupanua upatikanaji wa huduma za fedha na kuimarisha ujumuishaji wa fedha kwa kutoa suluhisho bunifu zinazounda thamani kwa wadau wote.
Robert Dommisse, Mkurugenzi Mtendaji wa Bima ya Maisha SanlamAllianz, alisema"Uzinduzi wa chapa ya SanlamAllianz Tanzania ni hatua muhimu kwa ushirikiano wetu pamoja na sekta ya huduma za fedha nchini.
Hii inaonyesha mkakati wetu wa kutumia utaalamu wetu katika masoko yanayokua, kuunda biashara zinazoongoza katika uchumi tunaoufanyia kazi, na pia inaunga mkono dhamira yetu ya kuwezesha watu wengi zaidi kupata huduma za fedha.
Kupitia ushirikiano huu, tunaweza pia kuunganisha nguvu na uwezo wa kimataifa wa Sanlam na Allianz. Kwa fursa kubwa za usambazaji, utaalamu na ushirikiano katika mawasiliano na bancassurance, tuna uhakika wateja wetu watanufaika na suluhisho bunifu za mahitaji yao.
"Jaideep Goel alisema "Kipaumbele chetu ni kutoa suluhisho za bima za jumla zenye kuaminika na za viwango vya kimataifa ambazo zinahifadhi kile kinachowajali zaidi watu na biashara nchini Tanzania.
Uzinduzi huu si tu kuhusu chapa mpya; ni kuimarisha ahadi yetu ya kusimama na wateja wetu katika kila hatua ya maisha na kila changamoto wanayokabiliana nayo.
"Julius Magabe aliongeza "Bima ya maisha ni kuhusu kujenga na kujiamini kwa ajili ya baadaye. Kupitia SanlamAllianz, tunaleta mchanganyiko wa utaalamu wa kimataifa na uelewa wa utalaamu wa ndani ili kusaidia Watanzania kupanga, kulinda, na kustawi.
Kipaumbele chetu kitakuwa kwenye bidhaa bunifu za bima ya maisha zinazochangia usalama wa fedha wa muda mrefu na ujumuishaji wa fedha."
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...