Na Khadija Kalili, Pwani
MSIMAMIZI wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo la Kibaha Mjini Bi.Theresia Kyara ametoa wito kwa wakazi wake kujitokeza kwa wingi ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025 kwa sababu ni haki yao ya msingi kupiga kura.
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 21 Oktoba 2025 , Kyara amesema kuwa vituo vitakua wazi kuanzia saa moja asubuhi hadi saa kumi jioni.
Kyara amesema kuwa Jimbo la Kibaha Mjini kuna Tarafa mbili, Kata 14, Mitaa 73 na vituo 467 vya kupiga kura.
Aidha amesema kuwa katika ngazi ya kuwania nafasi ya kiti cha Rais Vyama 17 vinawania huku nafasi ya Ubunge vyama 14 vinawania nafasi hiyo na kwenye nafasi ya Udiwani vyama vinne vimejitokeza kuwania.
Kyara amesema kuwa tangu kampeni zianze hadi sasa zinaendelea vizuri na hakuna malalamiko huku akiwasifia wagombea wote kuwa wanajeshimu ratiba zao za kampeni na hawajapokea malalamiko ya aina yoyote.
Wakati huohuo amesema kuwa Oktoba 25 Makarani wa uchaguzi watapewamafunzo huku wasimamizi wa uchaguzi wanapigwa msasa tarehe 26 na 27 pia kampeni zitafungwa tarehe 28 Oktoba 2025.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...