‎Handeni TC ‎ ‎

Hospitali ya Halmashauri ya Mji Handeni kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali Jhpiego na Pfizer Foundation wamezindua uchunguzi wa awali wa saratani ya matiti kwa wanawake ili kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa huo. ‎

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt. Hudi Muradi, amewataka wakazi wa Handeni kujitokeza kwa wingi kufanya uchunguzi wa saratani ya matiti na kusisitiza ugunduzi wa mapema ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara makubwa yanayosababishwa na kuchelewa kutambua ugonjwa huo. ‎ 

‎Kwa upande wake, Dkt. Rashid kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga – Bombo, ametoa elimu kuhusu dalili na viashiria vya awali vya ugonjwa wa saratani ya matiti kwa wanawake waliojitokeza katika Kituo cha Afya Kideleko, Handeni Mjini, akihimiza umuhimu wa uelewa wa jamii juu ya afya ya matiti. ‎ ‎

Naye, Dkt.Laurence Loitore kutoka Hospitali ya Halmashauri ya Mji Handeni ameishukuru Jhpiego kwa kutoa mafunzo ya kitaalamu ambayo yatasaidia kuongeza uwezo wa wataalamu wa afya katika kutoa huduma za uchunguzi wa saratani kwenye vituo vyote vya afya vya Halmashauri. ‎ ‎

Zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za Serikali kwa kushirikiana na wadau wa afya katika kupunguza vifo vinavyotokana na saratani ya matiti na kuimarisha huduma za uchunguzi na matibabu kwa wanawake nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...