NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), wadau wa kisiasa, na wananchi wamehimizwa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi kwa amani, uadilifu na uzalendo, ukiopangwa kufanyika Oktoba 29, 2025 nchini Tanzania.
Wito huu umetolewa leo, Oktoba 25, 2025, Jijini Dar es Salaam, na Mkuu wa Ujumbe wa Uangalizi wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Mkutano wa Kimataifa wa Ukanda wa Maziwa Makuu (FP-ICGLR), Rais Mstaafu wa Zambia, Mhe. Domitien Ndayizeye, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nchini kuanza rasmi jukumu la uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
“Tunaihimiza jamii ya Watanzania, hasa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, kushiriki kikamilifu, kwa amani na uwajibikaji, katika kuamua mustakabali wa taifa letu siku ya uchaguzi wa tarehe 29 Oktoba 2025. Uchaguzi huu ni fursa adhimu ya kuimarisha taswira ya Tanzania kama kisiwa cha amani, utulivu, umoja na ukomavu wa demokrasia katika Ukanda wa Maziwa Makuu,” amesema Mhe. Ndayizeye.
Aidha, ameitaka INEC kuendelea kuendesha mchakato wa uchaguzi kwa uwazi, weledi na kutokupendelea, ili kuhakikisha kila sauti ya Mtanzania inasikika na kuheshimiwa.
Mhe. Ndayizeye amesema uangalizi huu ni sehemu ya utekelezaji wa Itifaki ya ICGLR kuhusu Demokrasia na Utawala Bora, Mkataba wa Umoja wa Afrika juu ya Demokrasia, Uchaguzi na Utawala, pamoja na Sheria mpya za Uchaguzi za Tanzania za mwaka 2024.
Ujumbe wa FP-ICGLR utaangalia mchakato wa uchaguzi katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar, ikiwemo Mkoa wa Pwani, Dar es Salaam na Unguja. Uangalizi utazingatia hatua zote za mchakato wa uchaguzi kabla, wakati, na baada ya kupiga kura.
“Uangalizi utazingatia maandalizi ya taasisi zinazoratibu uchaguzi (INEC na ZEC), ushiriki wa wananchi hususan vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, mazingira ya haki za binadamu na usalama, uhuru wa vyombo vya habari, na hali ya jumla ya amani na ustahimilivu wa kisiasa nchini,” amesema Mhe. Ndayizeye.
Ujumbe wa FP-ICGLR unaundwa na wabunge na wataalamu 23 kutoka nchi sita wanachama wa CGLR: Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kenya, Tanzania na Zambia. Lengo kuu ni kuchangia juhudi za kikanda katika kukuza demokrasia, utawala bora, haki za binadamu, na maendeleo endelevu, sambamba na ahadi zilizowekwa na wakuu wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu chini ya Mkataba wa Amani, Usalama na Maendeleo wa mwaka 2006.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...