NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
KITUO Cha Taarifa na Maarifa katika kata ya Kitunda kimefanikiwa kuibua ajenda za kijamii na kuhamasisha usalama wa watoto wa kike pamoja na ushiriki wa wanawake katika uongozi, kufuatia kufanya tathimini ya mradi wa Women’s Leadership and Economic Rights (WLER).
Kituo hicho kimewezesha jamii kukubaliana na mpango wa kujenga uzio katika shule zote za kata hiyo ili kuwalinda watoto wa kike dhidi ya mazingira hatarishi, sambamba na kuwawezesha wanawake kushiriki katika nafasi mbalimbali za uamuzi na uongozi.
Akizungumza katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kituo hicho, Bi. Claudia Gabriel Kawonga, amesema mradi huo umeleta mabadiliko ya kimtazamo katika jamii, hasa katika kuthamini mchango wa wanawake.
“Baada ya kufanya tathimini ya mradi, tulipeleka mrejesho serikalini na kuanzisha mpango kazi tuliojiwekea. Tulizungumza na walimu, wazazi na viongozi wa mitaa, na wote tumekubaliana kwamba shule zetu ziwe na uzio ili kulinda watoto wetu,” amesema.
Bi. Claudia ameongeza kuwa kabla ya mradi huo, wanawake wengi walikuwa na hofu na dhana potofu kuhusu uongozi, lakini baada ya mafunzo na hamasa, baadhi yao wamepata nafasi za uwakilishi katika serikali za mitaa.
Kwa upande wake, Mwanaharakati wa masuala ya kijinsia wa kata hiyo, Bi. Mwajuma Kidulazi, amesema mradi wa WLER pia umechochea ufuatiliaji wa ajenda nyingine za kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara na uanzishwaji wa soko la kisasa katika kata hiyo.
“Barabara tayari tumeanza kuona utekelezaji kupitia serikali. Kuhusu soko, tumekubaliana baada ya uchaguzi kukamilika tukutane na mbunge atakayechaguliwa ili kuwasilisha rasmi changamoto hiyo,” amesema.
Licha ya hatua chanya zinazofikiwa nchini ikiwemo historia ya Tanzania kumpata Rais mwanamke kwa mara ya kwanza, wanawake wengi bado wanakabiliwa na changamoto zinazotokana na mfumo dume, umaskini na ubaguzi wa kijinsia.
Mradi wa WLER umeendelea kujikita katika kuhamasisha usawa wa kijinsia, kuwajengea wanawake ujasiri wa kushiriki katika maamuzi, na kubadilisha mitazamo inayowanyima fursa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...