Mkutano wa 30 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP30) unaotarajiwa kuanza Novemba 10-21,2025 kwenye jiji la Belém do Pará, nchini Brazil,umebeba fursa mpya ya Tanzania kusukuma agenda za mapambano dhidi ya uchafuzi wa bahari unaosababishwa na taka za plastiki hasa katika fukwe zilizopo kwenye mwambao wa Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Takwimu kutoka katika vyanzo mbalimbali likiwemo Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) vinabainisha kuwa jiji la Dar es Salaam, linazalisha wastani wa tani 4100 hadi 5,600 za taka ngumu kwa siku na ndilo linalochangia kiasi kikubwa cha taka hizo zinazoingia baharini.
Kutokana na umuhimu wa COP30 ambalo ni jukwaa rasmi la kimataifa kwa ajili ya kujadili na kuamua malengo ya kukataa uzalishaji wa hewa ukaa, kutafuta ufadhili wa fedha za kukabiliana na madhara ya mabadiliko tabianchi na kufikia makubaliano ya kimataifa yanayoathiri sera za kitaifa za utekelezaji wake kama vile mkataba wa Kyoto na Paris, Tanzania inayo nafasi ya kutafuta fedha za kukabiliana na changamoto ya taka ngumu zinazoingia baharini.
Ikumbukwe kuwa matokeo ya makubaliano hayo yanayofikiwa kwenye mikutano ya COP, yaliyoanza rasmi mwaka 1995 nchini Ujerumani yanagusa maisha ya kila siku ya mwananchi kupitia sera zinazoamuliwa na serikali kama vile miongozo ya nishati safi ya kupikia, ukarabati wa mazingira, mipango ya ujenzi wa miundombinu inayostahimili mabadiliko tabianchi na msaada kwa wakulima na wavuvi walioathika.
Mkutano wa mwaka huu ni mwendelezo wa mikutano hiyo inayofanyika kila mwaka tangu mwaka 1995 na msingi wake ni Mkutano wa Mazingira wa Dunia uliofanyika Brazili mwaka 1992 ambao uliridhia kuanzishwa kwa COP ambayo ni kifupi cha ‘Conference of the Parties’ unaohusisha wanachama wa UNFCCC-‘United Nation Framework Convention on Climate Change’, ambao ni mkataba wa kimataifa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi uliopewa jukumu la kuwa chombo cha utekelezaji na usimamizi wa mkataba huo.
CoP30 ni moja ya majukwaa muhimu zaidi duniani kwa majadiliano ya sera, mikakati na hatua za pamoja za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Kwa Tanzania, hii ni fursa adhimu ya kutafuta fedha zitakazosaidia kuwaongezea uelewa wa wananchi kuhusu nafasi ya nchi katika utekelezaji wa mikataba ya kimataifa, na kuhamasisha ushiriki wa jamii katika kulinda mazingira ya bahari na kukabiliana na athari mabadiliko tabianchi.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi licha ya kuchangia kidogo katika utoaji wa gesi joto (greenhouse gases). Hali hii imekuwa ikijitokeza kupitia mabadiliko ya mifumo ya mvua na ukame wa mara kwa mara, kupungua kwa upatikanaji wa samaki, uzalishaji wa chakula, kuongezeka kwa mafuriko, uharibifu wa miundombinu na magonjwa yanayosababishwa na mabadiliko tabianchi.

Katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mkutano huo wananchi hasa wakazi wa pwani ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam wanalo jukumu la kuhifadhi mazingira, kutambua sera na mikakati ya taifa kama vile Mkakati wa Kitaifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (NCCS), Mpango wa Taifa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kushiriki kikamilifu katika hatua za kijamii, kiuchumi na kiteknolojia zinazolenga kupunguza athari za tabianchi.
Umuhimu wa mkutano wa COP30 unafungua milango kwa serikali na wadau wa mazingira kufikisha elimu kwa wananchi mara kwa mara kwa kutumia redio, televisheni, magazeti na majukwaa ya kidijitali.
Ingawa umesalia muda mfupi wa kuelekea kwenye mkutano huo bado serikali na wadau wa mazingira wanayo nafasi ya kuzishirikisha jamii za vijijini kwa kuwapa elimu wakulima, wavuvi, wafugaji na wanawake kuhusu mbinu endelevu za uzalishaji zinazozingatia tabianchi sanjari na kufanya warsha na midahalo ya kijamii ili kubadilishana maarifa ya jadi na kisayansi.
Aidha ipo haja ya kuwajengea uwezo viongozi wa serikali za mitaa, mashirika ya kiraia (CSOs) na vyama vya wanahabari kuhusu maudhui ya COP30 na utekelezaji wa mikataba ya mazingira na kuanzisha mtandao wa mawasiliano unaounganisha sekta binafsi, mashirika ya kimataifa na serikali.
Katika mikakati ya muda mrefu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi serikali na wadau wanaweza kuongeza nguvu katika kuwatumia vijana waliopo shuleni kama injini ya mabadiliko kwa kuwapa elimu ya mabadiliko ya tabianchi katika mitaala ya shule na vyuo, kukuza ubunifu wa vijana kupitia miradi ya kijani, sayansi na teknolojia rafiki kwa mazingira na kuandaa mashindano ya kitaifa ya ubunifu kuhusu masuala mbalimbali ya uokotaji na urejezaji wa taka ngumu kwa kuzifanya fursa badala ya tatizo.
Pamoja na mambo mengine kuna haja kwa serikali na wadau kuanzisha kampeni zenye lengo la kuonesha hatua ambazo taifa limepiga katika kutekeleza ahadi za NDCs, kulikuwa na haja kuitisha mijadala ya kitaifa juu ya mabadiliko ya tabia nchi kabla ya mkutano wa Brazil ili kujadili vipaumbele vya Tanzania na kutoa sauti ya wananchi itakayowakilishwa kimataifa.
Aidha serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira ina wajibu mkubwa wa kuratibu juhudi za Wadau kama Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), TMF, Oxford Policy Management (OPM), Climate Action Network Tanzania (CAN),UNDP, WWF, na Tanzania Climate Change Forum hawa wanaweza kuendesha kampeni za kitaifa za uhamasishaji.
Ushirikiano wa sekta binafsi pia ni muhimu katika kuwekeza kwenye teknolojia rafiki kwa mazingira kama nishati jadidifu na urejelezaji wa taka ngumu.
Uelewa wa wananchi kuhusu COP30 na mabadiliko ya tabianchi si suala la kubembeleza bali ni hitaji la msingi la kitaifa. Kupitia kampeni madhubuti za kuiandaa jamii, mwenendo huu utaisaidia nchi kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kushiriki kikamilifu katika majadiliano ya kimataifa, kulinda maslahi yake ya kiuchumi na kijamii, na kuendeleza azma ya taifa ya “uchumi wa buluu” unaozingatia maendeleo endelevu.
Ripoti ya Mwongozo wa Kitaifa wa Kutambua Maeneo Hatari ya Plastiki na Kuunda Mikakati iliyooandaliwa na International Union for Conservation of Nature (IUCN) kwa kushirikiana na Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Mazingira (UNEP) na taasisi ya Life Cycle Initiative (chini mradi wa MARPLASTICCs), inabainisha kuwa, Jiji la Dar es Salaam linachangia zaidi ya asilimi 50 ya taka zote za plastiki zinazoishia kwenye mito, maziwa na baharini.
Kulingana na ripoti hiyo mwaka 2018 zaidi ya tani 29,000 ziliingia kwenye maji (bahari, mito na maziwa). Uchafuzi huu unatajwa kuzidisha athari za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo ya Pwani, huku umasikini wa wavuvi na wafanyabiashara wa samaki ukiongezeka.Kuelekea COP30, tuhamasike, tushirikiane, na tuwe sehemu ya suluhisho.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...