Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV-Bagamoyo 

WAKALA wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) pamoja na Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka (SLADS) wameingia mkataba wa makubaliano ya kushirikiana kutoa Mafunzo ya Muda mfupi kwa Watendaji na Watumishi wa sekta ya elimu.

Waliotia saini makubaliano ya mkataba huo ni Mtendaji Mkuu wa ADEM Dkt. Maulid Maulid na Kaimu Mkuu wa Chuo SLADS Bertha Mwaihojo.Mkataba huo umesainiwa Disemba 20,2025 wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Katika hafla hiyo ya utiaji saini mkataba umeshuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo SLADS.

Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa TLSB Dkt. Mboni Ruzegea, Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa TLSB Prof. Alli Mcharazo, Mkuu wa Chuo cha SLADS wa zamani Dkt. Alfred Nchimbi, Mkurugenzi wa Uendeshaji Huduma za Maktaba TLSB Dkt. Rehema Ndumbaro pamoja na menejimenti za TLSB na SLADS.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...