Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekuwa mshindi wa kwanza na kupewa tuzo ya umahiri katika utayarishaji bora wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2024 kwa kufuata viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu International Public Sectors Accounting Standards (IPSAS) katika kundi la Taasisi za Serikali zinazojitegemea.
Tuzo hiyo imetolewa tarehe 04/12/2025 na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA APC hotel Bunju jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Aretas Lyimo amekipongeza Kitengo cha fedha na uhasibu kwa kufanikisha uandaaji bora wa hesabu uliopelekea kuwa washindi wa tuzo hiyo.
"Niwashukuru watumishi wote wa Mamlaka hasa timu ya fedha na ukaguzi wa ndani kwa kujitoa, kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha kuwa taarifa zetu za fedha zinaandaliwa kwa kiwango cha juu kinachotambulika kimataifa. Tuzo hii ni matokeo ya kazi yao nidhamu, na ushirikiano ndani ya Taasisi'' amesema Kamishna Jenerali Lyimo.
Kamishna Lyimo ameongeza kuwa, ushindi wa tuzo hii ni ushahidi kwamba Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya inafuata na kuzingatia Sheria za fedha, Manunuzi na miongozi mbalimbali fedha inayotolewa na Hazina kwa nyakati mbalimbali.
Amesema, "DCEA inazingatia misingi ya uwazi, uwajibikaji na matumizi sahihi ya rasilimali za Umma inazopewa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. Ni heshima kubwa kwetu kutambuliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA)".
Pamoja na hayo ameongeza kuwa tuzo hii ni motisha ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kuhakikisha kuwa Mamlaka inaendeleza uwazi, uadilifu na usimamizi bora wa rasilimali walizopewa.
Hii ni mara ya nane DCEA kushinda tuzo hizi tangu mwaka 2017 na itaendelea kushirikiana na wadau wote ili kuhakikisha kuwa inatimiza majukumu yake kwa ufanisi na kwa manufaa ya watanzania wote.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...