KAMPUNI ya Sukari Kilombero imeingia katika ushirikiano wa miaka mitatu na Ifakara Bakery na Mpango wa Free Bread Fund, kwa kuchangia zaidi ya tani 23 za sukari ili kusaidia mpango wa kijamii unaotoa kifungua kinywa na mkate bure kwa makundi yenye uhitaji. Mpango huu unalenga kupunguza changamoto za upungufu wa chakula kwa wanafunzi wa shule na wagonjwa waliolazwa hospitalini.

Mpango wa Free Bread Fund ulianzishwa mwaka 2001 na unasimamiwa na Masista wa Shirika la Franciscan kupitia Ifakara Sisters’ Bakery, na umehudumia Wilaya ya Kilombero kwa zaidi ya miaka 24. Mpango huu kwa sasa unasaidia zaidi ya vituo 25, ikiwemo vituo vya watoto yatima, shule na hospitali, na kunufaisha vijana, yatima na wagonjwa wenye mahitaji mbalimbali.

Katika ushirikiano huu, Kampuni ya Sukari Kilombero itachangia zaidi ya tani 23 za sukari kwa kipindi cha miaka mitatu: 2025/26: kilo 6,000, 2026/27: kilo 8,000, 2027/28: kilo 9,000

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ifakara, Bw. Derick Stanley, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Sukari Kilombero, alisema:
“Tunajivunia kushiriki katika mpango huu kwa kuwa unalingana na dhamira yetu ya uwajibikaji kwa jamii tunazozihudumia. Mfano wa mpango huu unaendeshwa kwa uwazi na matokeo yanayopimika, hivyo ni rahisi kufikia walengwa wanaohitaji msaada zaidi.”

Aliongeza kuwa Kampuni ya Sukari Kilombero itaendelea kufuatilia na kutathmini matokeo ya mpango huu, huku ikitarajia kupanua wigo wa mpango ili kusaidia pia shule zinazozunguka Kiwanda chetu cha Sukari Kilombero, na hivyo kuimarisha elimu na ustawi wa jamii.

Sr. Senorina Lukwachala, mlezi wa mradi na kiongozi wa Masista wa Kanisa Katoliki, alitoa shukrani:

“Tangu kuanzishwa kwake, mpango huu umekuwa baraka. Awali mahitaji yalikuwa madogo na yalisaidiwa na familia kutoka Uingereza, lakini sasa mahitaji yameongezeka sana. Tunatoa shukrani za dhati kwa Kampuni ya Sukari Kilombero kwa kusaidia jambo hili la maana.”

Akimuwakilisha Askofu wa Jimbo Katoliki la Ifakara katibu wa jimbo Farther Ignas Kilolelo alisifu mpango huu akisema:

“Mpango huu unaonyesha dhamira yetu ya pamoja ya kuhudumia wenye uhitaji. Tunakaribisha ushirikiano zaidi kutoka kwa wadau kama Kampuni ya Sukari Kilombero ili kushirikiana kwa ajili ya lengo hili la heshima.”

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Ndg. Bi Pilly Kitwana akimwakilisha, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, alisifu ushirikiano huu: “Serikali inathamini wadau wanaoshiriki kutatua changamoto za kijamii. Msaada wa leo kutoka Kampuni ya Sukari Kilombero unaonyesha nguvu ya mshikamano katika kukabiliana na changamoto ngumu.”

Akipokea kilo 6,000 za sukari za awali kwa niaba ya wanufaika wa mpango huo, Bi. Nasra Juma kutoka Kituo cha kulea vijana cha elite day Care centre alisema: “Msaada huu umekuja kwa wakati muafaka na utatusaidia sana kuwezesha mazingira bora ya kujifunza. Tunakaribisha mipango kama hii kutoka kwa wadau wengine.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...