Matukio mbalimbali yaliyomhusisha Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb) wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara tarehe 11 Desemba 2025 ambapo amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Kenan Sawala pamoja na viongozi wengine wa Mkoa.

Katika ziara yake, Waziri Chongolo ametembelea Bandari ya Mtwara; Ofisi za Bodi ya Korosho; Kituo cha Tafiti za Kilimo cha TARI - Naliendele; Kongani la Viwanda lililopo Maranje; kituo cha wabanguaji wadogo wa Korosho kilichopo Mahuta, Tandahimba; kiwanda cha kubangua Korosho cha TANECU kilichopo Wilaya ya Newala.

Waziri Chongolo amewapa matumaini wakulima wa Korosho kwa kutoa salamu za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zilizoeleza kuwa “Serikali itaendelea kuwapunguzia mzigo wakulima wa Korosho kwa kuwa na uhakika wa pembejeo za kilimo.”

Ziara hiyo pia imehusisha wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo na baadhi ya Taasisi zake iliyoongozwa na Mha. Athumani Kilundumya, Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Umwagiliaji na Zana za Kilimo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...