Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kinaendesha semina ya siku tatu inayohusu uvumbuzi katika matumizi ya akili mnemba kwenye sekta ya usafirishaji na usimamizi wa mizigo. Semina hiyo imezinduliwa Desemba 16, 2025 na Rasi wa Ndaki hiyo, Prof. Cyriacus Binamungu, katika kituo cha Upanga.

Semina hiyo imewakutanisha wataalamu wa sekta ya usafirishaji, manunuzi na ugavi, walimu pamoja na wanafunzi wanaosomea taaluma zinazohusiana na sekta hizo. Lengo kuu la semina ni kuwapatia washiriki ujuzi na maarifa yanayoendana na maendeleo ya teknolojia ili kuboresha ufanisi wa sekta ya usafirishaji na usimamizi wa mizigo nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Prof. Cyriacus Binamungu aliwataka washiriki kutumia ipasavyo maarifa watakayoyapata ili kuimarisha sekta ya usafirishaji na usimamizi wa mizigo, hivyo kuwezesha ushindani na makampuni ya kimataifa pamoja na kuboresha huduma kwa wateja.

Prof. Binamungu aliwahimiza maafisa kutoka taasisi za umma, mashirika ya serikali pamoja na sekta binafsi kutumia ipasavyo maarifa wanayoyapata katika mafunzo hayo ili kuleta mabadiliko chanya katika utendaji wao wa kazi.

Aidha, alisema kuwa teknolojia ya akili mnemba imekuja kurahisisha utendaji kazi na kuboresha utoaji wa huduma kwa haraka, hivyo ni muhimu kuachana na utamaduni wa kufanya kazi kwa mazoea unaosababisha ucheleweshaji wa huduma.

“Teknolojia ya Akili Mnemba imekuja kurahisisha utendaji kazi na kutoa huduma kwa wakati. Acheni kufanya kazi kwa mazoea kwani dunia ya sasa imebadilika,” alisisitiza Prof. Binamungu.

Awali, akimkaribisha Rasi wa Ndaki hiyo, Mratibu wa Mradi wa Kuhne Foundation katika Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Omary Swalehe, alisema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo maafisa usafirishaji na ugavi katika matumizi ya Akili Mnemba ili kuwasaidia kuboresha taaluma na ufanisi wao kazini

Semina hiyo itakayodumu kwa siku tatu inawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya usafirishaji, usimamizi wa mizigo, manunuzi na ugavi. Semina hiyo imeandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam na kufadhiliwa na Taasisi ya Kuehne Foundation chini ya Mradi wa LEARN.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...