Na Mwandishi wetu, Ngorongoro.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imewawezesha wakinamama 84 kutoka Kata ya Ganako, wilayani Karatu, kufanya ziara ya mafunzo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro baada ya kupewa mafunzo ya kutengeneza majiko banifu ili kulinda mazingira
Ziara hiyo ni sehemu ya programu ya elimu kwa vitendo inayolenga kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na matumizi ya teknolojia rafiki na kuepuka kukata miti na matumizi ya mkaa kwa jamii inayozunguka hifadhi ya Ngorongoro.
Akizungumza katika ziara hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Bi. Lightness Kyambile, amesema hatua hiyo inalenga kuwawezesha wanawake kuwa mabalozi wa uhifadhi katika jamii zao ili kuepuka kukata miti, kuchoma mkaa na kuharibu mazingira.
Akina mama walioshiriki ziara hiyo wametoa shukrani kwa uongozi wa Ngorongoro kwa kuwapa nafasi ya kujifunza kwa vitendo na kuahidi kuendelea kutoa elimu hiyo kwa wanawake wengine katika vijiji vyao.
Ziara hiyo ya mafunzo imeandaliwa kwa kuwashirikisha Ganako Youth, ambao wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira na kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...