Wajumbe wa Baraza la OSHA wakifuatilia majadiliano mbalimbali yaliowasilishwa katika kikaocha Tano cha Baraza la Tano la wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika katika Ofisi za OSHA Jijini Dodoma.Desemba, 20, 2025.

*************

Na Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Bi.Mary Maganga, amesema Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ni Taasisi yenye umuhimu na nafasi kubwa katika kuwezeshashughuli za uzalishaji kufanyika kwa tija.

Ametoa kauli hiyo wakati akifungua Kikao cha Tano cha Baraza la Tano la Wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika leo (Desemba 20, 2025) JijiniDodoma ambapo Katibu Mkuu huyo alikuwa Mgeni Rasmi katika ufunguziwa kikao hicho.

Aidha, Katibu Mkuu huyo ameipongeza OSHA kwa kutekeleza ipasavyojukumu lake la msingi la usimamizi wa Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ambapo amewasisitiza watumishi kuendelea kufanya kazi kwaweledi kwa kadri ya kanuni za utumishi wa umma pamoja na kuimarishaushirikiano baina yao.

“Kabla ya kufungua rasmi kikao hiki, ninaomba nisisitize mambo machache; kwanza niwatake kufanya kazi kwa weledi kwani mara nyingitumekuwa tukiamini kwamba wito unahusiana na shughuli za viongozi wadini pekee lakini tunasahau kwamba hata hizi kazi zetu ni wito kwakuwakuna majukumu ambayo ni lazima tuyafanye kwa ajili ya watu ambaowanategemea sana huduma zetu,” ameeleza Bi. Maganga.

Awali akimkaribisha Katibu Mkuu kufungua kikao, Mtendaji Mkuu waOSHA, Bi. Khadija Mwenda, amesema kikao hicho kinalenga kutathminiutendaji wa Taasisi ya OSHA kwa kutazama kipindi kilichopita, kilichopo ilikupata mustakabali wa maendeleo ya OSHA katika kipindi kijacho.

“Kikao hiki pamoja na kutathmini utendaji wa Taasisi kwa mwaka wa fedhauliopita (2024/2025) kinalenga kuangalia mwenendo wa utendaji wetukatika miezi mitano iliyopita ya mwaka huu wa fedha (2025/2026) hususankatika kipindi hiki tunapoelekea kuandaa bajeti ya mwaka wa fedha ujao(2026/2027),” amesema Mtendaji Mkuu.

Alieleza kuwa kikao hicho kilitanguliwa na mafunzo kwa watumishi wote waOSHA katika masuala ya maadili ya utumishi wa umma, mpango mkakatiwa Taasisi wa miaka mitano ijayo (2026/2027-2030/2031), masuala ya afyaya akili pamoja na masuala ya itifaki.

Akiwasilisha salamu za wafanyakazi katika ufunguzi wa kikao hicho, NaibuKatibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE)ambacho wafanyakazi wa OSHA ni miongoni mwa wanachama wake, Bw. Rugemalila Rutatina, ameipongeza OSHA kwakuwa na utaratibu mzuri waushirikishwaji watumishi wote pasipo ubaguzi katika kufanya maamuzi yamasuala muhimu yanayohusu utendaji wa Taasisi hiyo.

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akitoa maelezo ya awali katika ufunguzi waKikao cha Tano cha Baraza la Tano la Wafanyakazi wa OSHA Kilichofanyika katika Ofisi za OSHA Jijini Dododma Desemba 20,2025.

Katibu Mkuu,Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Bi. Mary Maganga akihutubiakatika Kikao cha Tano cha Baraza la Tano la Wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika JijiniDodoma katika Ofisi za OSHA Desemba 20,2025.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Mahusiano, Bi.Mary Maganga akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya OSHA wakiongozwa na MtendajiMkuu, Bi. Khadija Mwenda katika kikao cha Tano cha Baraza la Tano la wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika Jijini Dodoma Desemba, 20, 2025.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE), Bw. Rugemalila Rutatina, akiwasilisha salamu za wafanyakazi katika Kikao cha Tano cha Baraza la Tano la Wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika Jijini Dodoma Desemba 20, 2025.

Wajumbe wa Baraza la OSHA wakiimba wimbo wa mshikamano (solidarity) wakati wa kikao cha Tano cha Baraza la Tano la wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika katika Ofisi za OSHA Jijini Dodoma Desemba, 20, 2025.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...