Na Khadija Kalili
JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Septemba hadi Novemba 2025 ambapo wamefanya misako ya kuzuia na kutanzua uhalifu katika Wilaya zote.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Pwani RPC Salim Morcas amesema kuwa katika operesheni hizo wamefanikiwa kukamata watuhumiwa 203 waliokutwa na makosa mbalimbali.

" Katika operesheni na misako hiyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limekamata Magobole 13 yaliyokuwa yanamilikiwa kinyume cha sheria,Bastola moja aina ya Luger M90 ikiwa na risasi tisa, Bunduki aina ya Shortgun moja , mitambo mitatu ya kupikia pombe ya moshi na pombe ya moshi lita 375" amesema Morcase.

Aidha amesema kuwa Jeshi hilo wamekamata dawa za kulevya aina ya bhangi viroba 21, debe tano , puli 557 kete 3998, misokoto 193,pakiti 43 za bhangi aina ya skanka vyote vikiwa na jumla ya kilogramu328.5 pia wameteketeza mashamba ya bhangi yenye ukubwa wa hekari4,Mirungi bunda 187 zenye jumla ya kilograms 187.

RPC Morcase amesema kuwa pia wamekamata Gari aina ya Scania lenye namba za usajili T.625 CBD na trela lenye namba T.467 lililobeba shehena ya nondo mali inayodhaniwa kuwa ya wizi.

Amesema kuwa katika operesheni hizo Jeshi la Polisi limefanikiwa kuokoa mali mbalimbali ambazo ni Pikipiki 37 za aina tofauti, Simu za Mkononi 93 za aina mbalimbali, Laptop moja na CPU moja,Bomba 28za Umeme, Ng'ombe 39, madumu 12 ya mafuta ya Dizel@20,mifuko 100 ya Saruji,Luninga tano za aina mbalimbali,vifaa mbalimbali vya nyumbani , magodoro mawili ,viatu jozi sita,vipande vitatu vya vitenge,vipande vitatu vya Khanga.

Vitu vingine vilivyokamatwa ni Madumu 206 ya mafuta ya kula aina ya Korie@lita 20,Mitungi ya gesi 15 ya aina mbalimbali, Radio nane , Sabufa na Spika zake na vipande 16 vya nyama ya pori.

Kamanda Morcase amesema kuwa katika makosa yaliyoripotiwa kwenye vituo vya Polisi, jumla ya kesi 47 zimefikishwa Mahakamani na kupata ushindi kwa huku watuhumiwa 53 wamehukumiwa vifungo mbalimbali Mahakamani ikiwemo vifungo vya maisha kwa makosa ya kubaka na kulawiti.

Wakati huohuo amesema kuwa Jeshi hilo limetoa Elimu ya Usalama barabarani ambapo Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limekamata jumla ya makosa 74,446 na kulipiwa faini za za papo kwa papo kiasi cha Shilingi 2,233,380,000

Aidha elimu hiyo ya usalama barabarani imetolewa katika Shule za Msingi 42,Shule za Sekondari 36 ,Vyuo vya Udereva viwili ambapo jumla ya wanafunzi 3234 wamepata elimu hiyo.

"Madereva na abiria katika stendi na vijiwe 54 vya bodaboda wamefundishwa matumizi sahihi ya alama za barabarani, haki na wajibu wa abiria na watembea kwa miguu huku jumla ya madereva 38 wamefungiwa leseni zao kwa makosa mbalimbali ya usalaam barabarani" amesema RPC Morcase.

" Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linatoa rai kwa wananchi kuendelea kulinda amani na utulivu kwa kufuata sheria na kanuni za nchi aidha katika kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka linawakumbusha wananchi wanaotarajia kusafiri kwenda Mikoa mbalimbali kwa kutumia vyombo vya moto na kuzingatia sheria za usalama barabarani na kutumia madereva wazoefu ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika na kusisitiza abiria kutosimama na wakishikwa mshtakiwa wa kwanz atakuwa abiria aliyesimama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...