Na.Ashura Mohamed- Arusha

MKUU wa Mkoa wa Mkoa wa Arusha CPA.Amos Makalla amesema juhudi zinahitajika katika kuhakikisha kuwa wananchi wengi wanajiunga na mfuko wa bima ya Afya kwa wote ili kuwa na uhakika wa Matibabu.

Rc Makalla ameyasema hayo leo Jijini Arusha,wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sheria ya Bima ya Afya wote inayotekelezwa na mfuko wa bima ya afya nchini (NHIF).

"Katika mkoa wa Arusha kuna Jumla ya wananchi Milioni 2,356,255 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022,ambapo wananchi laki 3,534,255 ndio pekee wamejiunga na wanatumia huduma za Bima ya Afya.

Amesema kuwa kila mtu ni mgonjwa mtarajiwa na wananchi wengi uwezo wao ni mdogo sana wa kupata matibabu

Alisema wananchi wengi wanachangangamoto ya matibabu lakini hawana bima kwaajili ya matibabu na Mkoa wa Arusha bado unamwamko mdogo wa uandishikishaji hivyo elimu zaidi inahitajika.

Amesema Mkoa wa Arusha wananchi 3,53,438 sawa na asilimia 15 ndio wamejiunga na bima ya afya kwa wote kati ya 2,356,255 .

"Bado kiwango cha watu kujiunga na mfuko huu ni kidogo hivyo tuna wajibu wa kuendelea kuhamasisha wananchi uhamasishaji inahitajika zaidi ili kuwezesha huduma za matibabu zinazotolewa kupitia bima ya Afya"

Aidha amesema ni wajibu sasa wadau mbalimbali kuhakikisha asilimia 85 iliyobaki inaelimishwa ili wajue umuhimu wa bima hiyo kwasababu hujui kesho yako itakuwaje pale utakapoumwa.

Amesema elimu hiyo ifike katika makundi mbalimbali wakiwemo mamalishe, bodaboda, wananchi wanaoishi vitongoji na mitaa ili wajue umuhimu wa kujiunga na mfuko huo wa bima ya afya kwa wote

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dk, Charles Mkombachepa amesisitiza elimu hiyo ni muhimu kutolewa kwa wananchi wote ili wajue umuhimu wa kujiunga na mfuko huo kwa lengo la kupata matibabu pale wanapoumwa

"Mfuko huo una lengo la kuwaponya wananchi pale wanapochangia na kutibiwa pale watakapopata changamoto za afya"Amesisitiza Mganga Mkuu

Wakati huo, Mwenyekiti wa Mamalishe Mkoa wa Arusha, Hilda Stephen amempongeza Rais Samia kwa kuona bima hiyo inafaa kwa wote hivyo wataenda kutoa elimu kwa wananchi kujiunga na bima hiyo ili wapate matibabu

"Tunaisubiri kwa hamu hii ya afya kwa wote ili tupate matibabu kwani sisi mamalishe vipato vyetu ni vya chini hivyo endapo tukijiunga na mfuko huu tutaokoa maisha yetu na familia zetu pale wanapougua"Amesema bi Hilda

Bw.Miraji Kisile ni Afisa Uanachama (NHIF),amesema kuwa mwamko kwa wananchi bado ni mdogo licha ya elimu mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa kwa wananchi katika nyakati tofauti tofauti.

Kisile amesema kuwa ujio Mpya wa Sheria ya kila mwananchi kujiunga na mfuko huo,pamoja na mikakati na njia madhubuti zitarahisisha na kuwezesha wananchi wengi kujiunga na Mfuko huo.
Miraji Kisile Afisa Uanachama NHIF Mkoa wa Arusha





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...