Na Mwandishi Wetu,Arusha
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imezindua rasmi kampeni ya msimu wa sikukuu “ Funga mwaka kijanja Talii ( season two)” ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za Serikali kuhamasisha utalii wa ndani na kuongeza ushiriki wa Watanzania katika kutembelea vivutio vya taifa lao, hususan kipindi cha mwisho wa mwaka.
Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika leo, Desemba 15, 2025 jijini Arusha, ukiongozwa na Mkurugenzi wa Masoko wa TTB, Ernest Mwamwaja kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya umma na binafsi wanaojihusisha na uandaaji wa vifurushi vya safari, kwa lengo la kuwapatia Watanzania fursa nafuu na zilizoboreshwa za kutalii ndani ya nchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mwamwaja amesema kampeni hiyo inalenga kuwahamasisha wananchi kutumia kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka kutembelea Hifadhi za Taifa, eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, mapori ya akiba, hifadhi za misitu, maeneo ya urithi wa dunia pamoja na Makumbusho ya Taifa, huku wakichangia kukuza uchumi wa taifa na kuongeza ajira kwa wananchi.
Amefafanua kampeni hiyo inatekelezwa chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia taasisi zake zikiwemo TANAPA, NCAA, TAWA, TFS na Makumbusho ya Taifa, kwa kushirikiana na sekta binafsi,” amesema Mwamwaja.
Kwa upande wake, Ofisa Utalii wa TAWA Makuyuni, Mustapha Bulegera, amesema kampeni hiyo inatoa fursa kwa wananchi kufurahia vivutio vya asili vilivyopo nchini ikiwemo wanyamapori, mandhari ya kuvutia na urithi wa kiutamaduni.
“Wakazi wa Dar es Salaam watapata nafasi adhimu ya kuwaona wanyamapori hai katika viwanja vya Sabasaba kwa gharama nafuu, kampeni ya funga mwaka kijanja - talii itafungwa rasmi Januari 10, 2026.”



.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...