Na Editha Karlo,Kigoma.

WAANDISHI wa Habari wa Mkoa wa Kigoma toka vyombo mbalimbali wamefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo 14 kati ya miradi 57 inayotekelezwa na Manispaa ya Kigoma ujiji.

Ziara hiyo ambayo iliongozwa na mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma ujiji Kisena Mabuba alisema kuwa Manispaa inatekeleza miradi 57 yenye thamani ya zaidi Bilioni 53 fedha toka serikali pamoja na makusanyo ya mapato ya ndani.

Mkurugenzi alisema miradi yote 57 imeshaanza kutekelezwa huku baadhi ya miradi imekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi ikiwemo ofisi za watendaji wa kata na hospital ya Manispaa ambayo imeanza kutoa huduma.

"Ziara kama hii itaendelea kwa makundi mengine ili wananchi wajue miradi inayoendelea kutekelezwa kutokana na kodi zao,kundi litakalofuata kutembelea miradi baada ya nyie ni viongozi wa wafanyabiashara,viongozi wa dini na wazee maarufu"alisema Mkurugenzi

Kwa upande wake ofisa Elimu msingi wa manispaa ya kigoma Richard Mtauka amesema idara ya elimu ya manispaa ya kigoma imepokea sh 2.5 bilioni kwaajili ya ujenzi wa shule 13 zikiwemo shule nne mpya.

Alisema halmashauri ya Kigoma ujiji ina jumla ya shule za msingi 47 na ina jumla ya wanafunzi 51,892,huku kukiwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 596 hivyo ujenzi wa shule hizo mpua utasaidia kupunguza changamoto ya zote katika shule.

Naye Mkuu wa idara ya mipango na uratibu(mchumi)wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma ujiji Julius Ndele amesema jumla ya miradi 14 imetembelewa na waandishi wa habari ambapo shilingi bilioni 51.6 ni pesa toka serikali kuu na shilingili bilioni 2.1 ni kutokana na mapato ya ndani.

Baadhi ya wananchi waliongea na mwandishi wa habari hii wamesema kuwa utekezaji wa miradi hiyo ya kimkakati katika Manispaa ya Kigoma Ujiji itafungua uchumi wa manispaa na mkoa kiujumla pia itasaidia kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi.

"Tunamshukuru Rais wetu Dkt Samia kwa kuinfungua kigoma kwa miradi mikubwa ya kimkakati ambayo inatugusa wananchi moja kwa moja uongozi wake umeacha alama kwa mkoa wetu wa Kigoma"alisema Racher Charles mfanyabiashara wa soko la seremala kigoma mjini.

Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi unaondea wa shule mpya za awalu na msingi kata ya kibirizi na Buhanda,upanuzi wa uwanja wa ndege kigoma,ujenzi wa kituo cha afya Rusimbi,ofisi ya kata ya kasimbu,ujenzi wa barabara ya Bangwe-Ujiji.

miradi mingine waliyotembelea waandishi wa habari ni ujenzi wa daraja la mto Ruiche,Hospital ya Manispaa ya Kigoma ujiji,ujenzi wa ukumbinwa kisasa,ujenzi wa soko la kisasa na ujenzi wa jengo la utawala unaoendelea.

Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Mipango na Uratibu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, Julius Ndele alisema kuwa katika ziara hiyo ambapo waandishi wa habari walitembelea miradi 14 ni sehemu ya miradi 57 ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 51.7 Kimetolewa na serikali kuu na shilingi Bilioni 2.1 ni kutokana na mapato ya ndani.
Ujenzi wa daraja la Ruiche lililopo katika kata ya Kagera ukiendelea hii itawasaidia wananchi kutokana na adha ya kuvuka mto kwa kutumia viboti vidogo kufuata huduma upande wa pili
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Kisena Mabuba akiongea na waandishi wa habari katika eneo la mwanga linapojengwa soko la kisasa ikiwa ni moja ya miradi 57 inayotekelezwa
Baadhi wa waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma wakiwa sambamba na mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma ujiji kutembelea miradi inayotekelezwa na halmashauri ya manispaa hiyo

Mradi wa ujenzi wa kituo cha afya ya Rusimbi ukiendelea kituo ambacho kitasaidia kusogeza huduma za afya kwa wananchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...