Serikali wilayani Bukombe imefanya hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za Msingi katika wilaya hiyo ambapo wilaya hiyo imekuwa ya kwanza katika halmashauri 6 za mkoa wa Geita kwa kufaulisha wanafunzi kwa asilimia 86.37% darasa la 7.
Akitoa taarifa ya ufaulu wilayani humo afisa elimu awali na msingi Marycelina Coelestine Mbehoma amesema kuwa ufaulu huo ni ongezeko la asilimia 9.37% ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2024.
Kwa miaka mitatu mfululizo halmashauri hiyo ilikuwa ikishuka katika asilimia za ufaulu wa mitihani ya darasa la 7 hali iliyokuwa ikiisononesha Idara ya Elimu ya awali na msingi hivyo kuweka mikakati madhubuti iliyosaidia kupanda kwa matokeo ya mwaka 2025.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe bi Adelina Mfikwa amewataka walimu katika halmashauri hiyo kufanya majukumu yao ya serikali kikamilifu ili kutimiza malengo ya kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
Bi Mfikwa alisema kuwa katika halmashauri hiyo ni mwalimu hatakiwi kufanya shughuli za bodaboda, ulevi pamoja na utoro mashuleni ili kusimamia majukumu yao kikamilifu.
"Ninatambua kama mwajiri ninatambua kuwa wapo walimu ambao hawatimizi wajibu wao, kuna wengine nimewaona ni bodaboda, inawezekana wenyewe hawajui kama mimi nafahamu lakini nafahamu wanaendesha bodaboda, wapo walevi, wapo watoro, mimi nataka mtu afanye kazi na atimize wajibu wake" alisema Mfikwa.
Aidha katika kupambana na utoro mashuleni katika wilaya ya Bukombe mkuu wa wilaya ya Bukombe Paskasi Muragili ameagiza kukamatwa kwa mzazi ambaye mtoto wake atafikisha siku 14 bila kuwepo shuleni.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya idadi ya watoto wanaokatisha masomo bila sababu za msingiili kuongezeka hivyo ili kupunguza idadi hiyo hatua mkuu wa wilaya hiyo ametoa maelekezo.









Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...