Benki ya Absa Tanzania leo imehitimisha rasmi kampeni yake ya 'Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa' iliyodumu Kwa miezi mitatu baada ya kufanyika kwa droo ya tatu na ya mwisho katika hafla Iliyofanyika jijini Dar es Salaam, jana.
Droo ya mwisho imehitimisha kampeni ya miezi mitatu iliyolenga kuwazawadia wateja kwa kufanya miamala na huduma za kibenki kwa njia za kidijitali ikiwa ni pamoja na matumizi ya kadi, huku ikithibitisha dhamira ya Absa ya kuhimiza miamala salama, rahisi na isiyotumia fedha taslimu.
Katika hafla hiyo, Absa ilifanya droo ya mwisho ya kila mwezi na kutoa jumla ya shilingi milioni 18 za Kitanzania (TZS 18 milioni) kwa wateja watatu walioibuka washindi kutokana na ushiriki wao katika mwezi wa mwisho wa kampeni.
Washindi hao ni Bw. Abdulrazak Ali Seif (TZS 10 milioni), Bi. Aysha Mbarak Meghji (TZS 5 milioni), na Bw. Gibbons Samuel Katule (TZS 3 milioni). Droo hiyo ilifanyika kwa kuzingatia Masharti na Vigezo vya kampeni na mbele ya mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, ili kuhakikisha uwazi na haki katika mchakato wa uchaguzi wa washindi.
Katika tukio lililosubiriwa kwa hamu zaidi wakati wa kilele cha kampeni hiyo, Bi. Nasreen Karim Abdallah aliibuka Mshindi wa Zawadi Kuu, akiondoka na shilingi milioni 30 za Kitanzania (TZS 30 milioni). Ushindi huo umetokana na matumizi yake ya mara kwa mara ya huduma za benki za kidijitali na kadi za Absa katika kipindi chote cha kampeni, na unaonesha jinsi miamala ya kila siku inaweza kuleta mabadiliko makubwa katika maisha.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga, alisisitiza mchango mkubwa wa wateja katika mafanikio ya kampeni hiyo:
“Kampeni hii imekuwa na Manufaa mkubwa kwa wateja wetu tangu mwanzo. Tumehamasishwa kuona jinsi wengi wao wakichangamkia njia rahisi, salama na zisizotumia fedha taslimu katika kufanya miamala. Play Your Cards Right imeonesha kuwa pale wateja wanapochagua benki ya kidijitali, kila mtu hunufaika, kuanzia urahisi wa huduma hadi kuimarika kwa ujumuishaji wa kifedha.
"Tunawashukuru kwa dhati wateja wetu kwa kuendelea kuiamini Absa na kuwa sehemu ya safari hii.”
Kwa upande wake, Mkuu wa Usimamizi wa Taarifa na Uchambuzi wa Takwimu (MI & Analytics), Bw. Denis Kessy, alieleza athari pana ya kampeni hiyo:
“Absa tunaamini kuwa kila mteja ana Stori yenye thamani. Kampeni hii imetupa fursa ya kusherehekea Stori hizo, kubwa na ndogo, kwa kuwazawadia wateja wetu kwa kutumia tu huduma zetu za benki.
Tunapohitimisha kampeni hii leo, tunajivunia si mshindi wa zawadi kuu pekee, bali kila mteja aliyeshiriki.”
Aliendelea kusisitiza ukubwa wa mafanikio ya kampeni hiyo kwa kusema:
“Kupitia kampeni hii, Absa iliwazawadia washindi 72 wa kila wiki, washindi tisa wa kila mwezi na mshindi mmoja wa Zawadi Kuu, kwa jumla ya shilingi milioni 120 za Kitanzania (TZS 120 milioni) zilizorejeshwa kwa wateja wetu.
Huu ni uthibitisho dhahiri kuwa kuchagua Absa kunalipa.”
Kampeni ya Play Your Cards Right ilikuwa kampeni ya zawadi kwa wateja iliyodumu kwa miezi mitatu kuanzia Oktoba hadi Desemba 2025, ikiwa na lengo la kuhamasisha matumizi ya malipo ya kidijitali na yasiyotumia fedha taslimu. Wateja walipata nafasi ya kushiriki katika droo za kila wiki na kila mwezi kwa kutumia kadi zao za debit au credit za Absa kupitia malipo ya kuswipe, kutap (tap) au ununuzi mtandaoni.
Kwa kukamilika kwa droo ya mwisho, kampeni ya Play Your Cards Right imefikia tamati rasmi. Washindi waliotangazwa katika droo ya mwisho watatambuliwa rasmi katika hafla maalum ya kukabidhi zawadi itakayofanyika mwezi Februari, na hivyo kuhitimisha kampeni hii kwa namna ya kukumbukwa, ikiwa ni uthibitisho wa dhamira ya Absa ya kuwaweka wateja katikati ya kila zawadi na kila hatua ya safari yake.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki yaAbsaTanzania, Bw. Aron Luhanga (kushoto), akifanya droo ya mwisho ya kampeni ya benki ya miezi mitatu ya 'Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa', jijini Dar es Salaam jana. Mteja wa benki hiyo, Bi. Nasreen Karim Abdallah, alijinyakulia zawadi kuu ya Tsh 30,000,000. Kampeni hiyo ililenga kuwahamasisha wateja kuongeza matumizi ya kadi za debit na credit za Absa pamoja na huduma za kibenki kwa njia za kidigitali za benki hiyo.
Mmoja wa washindi wa kila mwezi wa kampeni ya miezi mitatu ya benki ya Absa Tanzania iitwayo 'Ujanja ni Kuswipe na Benki ya Absa' Bw. George Kivaria, akichukua tiketi ya bahati nasibu ili kumpata mshindi wa droo Kuu wakati wa droo ya mwisho iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Mteja wa benki hiyo, Bi. Nasreen Karim Abdallah, alishinda zawadi kuu ya Tsh 30,000,000. Kampeni hiyo ililenga kuwahamasisha wateja kuongeza matumizi ya kadi za debit na credit za Absa pamoja na pamoja na huduma za kibenki kwa njia za kidigitali za benki hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga.
Mkuu wa Usimamizi wa Taarifa na Uchambuzi wa Takwimu wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Dennis Kessy (wa tatu kushoto), akikabidhi hundi ya mfano ya Tsh 500,000/- kwa Bw. George Kivaria (wa pili kushoto), mmoja wa washindi wa kampeni ya miezi mitatu ya benki hiyo iitwayo 'Ujanja ni Kuswipe na Benki ya Absa' wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kampeni hiyo ililenga kuwahamasisha wateja kuongeza matumizi ya kadi za debit na credit za Absa pamoja na huduma za kibenki kwa njia za kidigitali za benki hiyo.
Mkuu wa Usimamizi wa Taarifa na Uchambuzi wa Takwimu wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Dennis Kessy, akikabidhi hundi ya mfano ya Tsh 500,000/- kwa Bw. Mohammed Zulfikar Hemani (kushoto), mmoja wa washindi wa kampeni ya miezi mitatu ya benki hiyo iitwayo 'Ujanja ni Kuswipe na Benki ya Absa', wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...