Airtel Yaongeza Upatikanaji wa Mawasiliano kwa mikoa ya  Singida, Dodoma na Shinyanga Kupitia Uzinduzi wa Minara Minne ya MawasilianoTanzania, 15 Januari 2026 – Airtel Tanzania imezindua minara minne mipya ya mawasiliano katika Mikoa ya Singinda - Mugungia (mnara 1), Dodoma - Mpunguzi  (minara 2), na Shinyanga - Ngokoro (mnara 1), hatua iliyoboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano  na intaneti kwa wananchi wanaoishi maeneo hayo. Miundombinu hii mipya ni sehemu ya uwekezaji endelevu wa Airtel katika kupanua huduma za mawasiliano ya kuaminika kote nchini, hususan katika maeneo yaliyokuwa hayajahudumiwa vya kutosha.

Akizungumza wakati wa haflaya uzinduzi iliyofanyika Dodoma, Diwani wa Kata ya Mpunguzi, Isaya Aidan, aliishukuru Airtel kwa kuwekeza katika eneo hilo, akibainisha kuwa mnara huo utakuwa kichocheo cha maendeleo ya haraka. Aidha, aliwataka vijana wa Mpunguzi kutoendelea kubaki nyuma.
“Huu ni wakati wa vijana kuchangamkia fursa. Uwepo wa mtandao imara hapa Mpunguzi unafungua milango ya biashara za kidijitali, huduma za kifedha, na ajira. Msisubiri anza kutumia fursa hizi sasa ili kuleta maendeleo binafsi,” alisisitiza.
Mkoani Singida, mnara mpya utabiresha mawasiano na kuchichochra kukua kwa sekta ya biashara hasa kwa wakulima wa alizeti, ambao kupitia mnara huu watawasiliana na wateja wao, watapokea pesa na kutuma pesa na wataweza kupata fursa mpya za kidijitali .
Wakati wa uzinduzi uliofanyika Ngokoro, Shinyanga, Meneja wa Kanda wa Airtel, Bw. George Mwakabungu, alieleza athari chanya za mnara huo katika maisha ya kila siku na maendeleo ya jamii.


“Mnara huu utaboresha kwa kiasi kikubwa mawasiliano katika eneo la Ngokoro. Wananchi sasa wataweza kupiga simu kote nchini, kutumia huduma za fedha kidijitali, na kupata intaneti kwa urahisi, Mnaea huu urahisisha shughuli za kibiashara na kuboresha upatikanaji wa taarifa,” alisema Bw. Mwakabungu.
Kwa upande wake, mkazi wa Mbungia, Singida, alieleza furaha yake akisema:
 “Huu ni wakati muhimu kwa jamii yetu. Kupatikana kwa mtandao wa Airtel hapa Mbungia kunafungua fursa mpya kwa wafanyabiashara wa ndani kukua zaidi ya mauzo ya ana kwa ana. Kupitia mtandao wa uhakika, sasa tunaweza kutangaza bidhaa zetu kidijitali, kuuza mtandaoni, na kufikia masoko mapana zaidi ili kuboresha maisha yetu.”


Airtel Tanzania inaendelea kuweka kipaumbele katika upanuzi wa mtandao kama sehemu ya dhamira yake ya kukuza ujumuishi wa kidijitali, kuhakikisha jamii kote nchini zinapata huduma za mawasiliano ya simu na intaneti zilizo bora, nafuu, na za kuaminika. Kupitia uwekezaji endelevu wa miundombinu, Airtel inaendelea kuwaunganisha watu, kuwezesha jamii, na kuunga mkono maendeleo ya taifa.


“Upanuzi huu wa mtandao utawezesha jamii za Mbungia na maeneo jirani kuendelea kuwasiliana, kupata huduma za kifedha kwa njia ya simu, na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali,” alisema.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...