Na. Vero Ignatus, Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Jiji Joseph Mkude amewataka waendesha bodaboda kuchangamkia fursa za mikopo ya pikipiki zinazotolewa akisisitiza nidhamu ya matumizi ya fedha ili waweze kuwa waaminifu na kurudisha mikopo hiyo kwa Muda sahihi.
Akizungumza hivi karibuni katika uzinduzi wa zoezi la utoaji wa pikipiki za mikopo chini ya udhamini wa Kampuni ya VTS, Mkude amesisitiza ili waweze kuwa wamiliki halali wa vyombo vyao,kuongeza kipato na kufanya biashara zao kwa uendelevu. mikopo irejeshwe kwa wakati , lazima suala la uaminifu lizingatiwe kustahili mikopo zaidi siku zijazo.
Sambamba na hilo Mkude , amewataka wananchi kujiunga na bima ya afya, kwahi husaidia kupata huduma Bora za matibabu bila gharama kubwa,hivyo ni wakati wa kila mmoja kwanza na Bima ya Afya pamoja na kushirikiana .katika usafirishaji, na kushirikiana katika miradi ya maendeleo ya kijamii.
"Sasa ni wakati wa kila mmoja kuanza na bima ya afya Tukikusanya nguvu, tutakuwa imara zaidi kama jamii, Tusisimame tulipo, bali tuendelee mbele ,ni lazima tushirikiane katika kila hatua, hasa katika miradi ya afya na usafi wa mazingira na nisisitize mshikamano na ushirikiano katika miradi ya kijamii ni msingi wa maendeleo endelevu” alisisitiza.
Vilevile amelitaka Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani kuhakikisha waendesha pikipiki wanapatiwa mafunzo na leseni, hasa kwa wale wasio na leseni, ili kuongeza uelewa wa sheria za usalama barabarani na kupunguza ajali.
Mkude pia aliwaonya baadhi ya vijana wanaojihusisha na biashara ya pikipiki zisizo rasmi,na kuwataka kuhakikisha wanazingatia taratibu na sheria ili kulinda usalama wa watumiaji na taswira ya sekta ya usafirishaji.
“Tusisimame tulipo, bali tuendelee mbele ,ni lazima tushirikiane katika kila hatua, hasa katika miradi ya afya na usafi wa mazingira na nisisitize mshikamano na ushirikiano katika miradi ya kijamii ni msingi wa maendeleo endelevu” alisema.
kwa upande wake katibu wa bodaboda Wilaya ya Arusha mjini Richard Magembe, alishukuru sana serikali kwa namna inavyotambua mchango wa kundi la bodaboda katika kukuza uchumi wa wananchi na kusema kuwa wapo tayari kushirikiana nayo na wadau wengine wakati wowote watakapohitajika.
Umoja wa bodaboda wilaya tumelipia keshi pikipiki 12 zenye thamani ya milioni 36.
Kisha kampuni ya TVS ikakopesha umoja pikipiki 10 Hivyo jumla zinakuwa pikipiki 22 Ambazo umoja wa bodaboda unawakopesha wanachama kwa mikataba nafuu. Alisema Maghembe.
Aidha alibainisha mafanikio yao, ikiwemo kupata shilingi milioni 20 kutoka kwa wadau wa maendeleo zilizotumika kuanzisha shughuli za kiuchumi na kuboresha ustawi wa wanachama, pamoja na kufungua akaunti katika kata zote 25 za Wilaya ya Arusha Mjini kuhifadhi michango na akiba.
Mkutano huo ulihitimishwa kwa wito wa mshikamano, uwajibikaji, na mshikamano miongoni mwa wananchi, huku viongozi wa serikali na wadau wa usafirishaji wakiahidi kushirikiana zaidi katika miradi ya maendeleo ya kijamii.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...