Na. Emmanuel Buhohela, Dodoma
Kamati ya kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Serikali kwa kutatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya upungufu wa Watumishi katika Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Thimotheo Mzava Jijini Dodoma wakati kamati hiyo ikipewa mafunzo kuhusu Muundo na majukumu ya Wizara na Taasisi zake na kutaka jitihada hizo kuendelezwa ili kuwa na uwiano mzuri wa watumishi katika Taasisi ili ziweze kutekeleza kikamilifu majukumu yake.
Mhe. Mzava ameongeza kuwa kwa kipindi kilichopita kamati hiyo imekuwa ikipokea malalamiko ya upungufu wa watumishi tofauti na hali ilivyo sasa na kuiopongeza Serikali na kwamba Kamati hiyo ya kudumu ya Bunge inatarajia kuimarika kwa utendaji
Aidha, ameitaka wizara kuendekea kuvitazama na kuviwezesha vyuo vilivyoko chini ya wizara ili kuviwezesha kuzalisha wataalam na kutoa mchango katika sekta ya ajira.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo waliopata fursa za kutoa ushauri na maelekezo wamesema wako tayari kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuendeleza uhifadhi ili kizazi kijacho kiweze kunufaika na rasilimali hiyo adhimu.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha kikao cha leo Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema Serikali inaendelea kuwa sikivu na kutekeleza majukumu yake ya kusimamia kikamilifu na kuendeleza sekta ya uhifadhi na Utalii ili kuwanufaisha wananchi wote.
Ameongeza kuwa kutokana na kauli mbiu ya chama cha mapinduzi ya kazi na utu Wizara itaendelea kutekeleza majukumu yake ipasavyo ili kufikia maono ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuacha tabasamu kwa wananchi pindi atakapomaliza muhula wake wa uongozi. Tanzania
Taasisi zilizowasikisha taarifa zake kwa niaba ya Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii ni Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Chuo Cha Usimamizi wa Wanyamapori (MWEKA) pamoja na Chuo Cha Taifa cha Utalii (NCT).
Kikao hicho kimeongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Thimotheo Paul Mzava (Mb) na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb.), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu Bw. Nkoba Mabula, Menejimenti ya Wizara, Wakuu wa Taasisi pamoja na vyuo vilivyopo chini ya Wizara.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...