Mwenyekiti Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Bw. Eric Shitindi amekutana na wasimamizi wa sheria mbalimbali katika kituo cha Mpaka cha Mutukula, Kagera tarehe 29 Januari, 2026 na kuteta kuhusu masuala ya udhibiti wa bidhaa za dawa na vifaa tiba katika kituo hicho.
Akizungumza na watendaji hao, Mwenyekiti alisema lengo la zuara hiyo ni kujionea shughuli za kiudhibiti maeneo ya Mpakani ba kujifunza changamoto zilizopo ili kushauri namna ya kuzitatua.
" Serikali ni moja na yote yanayofanyika yanalenga kuhudumia wananchi, hivyo rai yangu ni kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto za mipakani" , alisema Bw. Shitindi.
Akitoa taarifa ya utendaji wa kituo, Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Forodha cha Mutukula, Bw. Lubinza Edmund, alisema kituo hicho kina taasisi 20 za udhibiti na jumla ya watumishi ni 116 ambao hufanya kazi kwa ushirikiano katika kubaini magendo na kukabiliana nayo ili kuhakikisha soko la Tanzania linakuwa salama kwa mujibu wa sheria zilizopo.
Bw. Lubinza aliendelea kuainisha changamoto nyingine kuwa ni ukubwa wa Mpaka ambao una vipenyo vingi, jambo ambalo ni hupelekea bidhaa kuingia kwa kificho hivyo ni lazima watendaji kushirikiana muda wote.



.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...