Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema Mabalozi wa Mashina ndiyo nguzo ya kukipambania Chama,Kwani ndiyo macho, masikio na daraja la kuunganisha Chama Cha Mapinduzi na kuendelea kulinda umoja wao kama nguvu ya kusonga mbele ili kuwatumikia wananchi.
Akizungumza leo Januari 20,2026 katika Mkutano wake na Mabalozi wa Mashina Mkoa wa Dodoma, Dkt Migiro amesema Mashina ni ngome ya ulinzi wa chama kwani yataendelea kuwa Walezi, na kuwaunganisha wananchi pamoja, kwani siasa Lazima iende sambamba na uchumi ndio maana Mashina yanatija kwa Chama.
Amesema ni mahala pa kuikusanya jamii pamoja, kutangaza kazi nzuri inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka kufanya vikao vya mara kwa mara na kufikisha maadhimio ngazi za juu, ambapo kupitia Chama wanaweza kuishauri serikali iliyoko madarakani.
Dkt. Migiro ametoa wito kwa viongozi wa ngazi zote za Kitaifa, kuhakikisha wanahudhuria vikao vya Chama kwenye ngazi za Mashina, ili kujadili kwa pamoja na kutatua au kueleza ahadi walizoahidi watakaposhika Dola zimefikia wapi utekelezaji wake, ili kulinda umoja wa Chama na kuwa nguvu ya kusonga mbele kuwatumikia wananchi.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Wabunge waliohudhuria mkutano huo, Mbunge wa Jimbo la Mtumba na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde, amesema kuwa katika miaka mingi iliyopita hakuna kipindi ambacho Chama kimewaangalia Mabalozi vizuri kama awamu hii ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, akitoa rai kwa Mabalozi na viongozi wote kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Katibu Mkuu.




















Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...