Na Mwandishi Wetu

Hatua kubwa ya mageuzi ya kodi nchini imefikiwa kufuatia tangazo la kuanza kutumika kwa mfumo mpya wa ukusanyaji wa kodi za ndani, hatua inayotarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya mapato ya Serikali.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bwana Yusufu Mwenda, amesema mfumo huo utaanza rasmi kutumika Februari 9, 2026, baada ya Serikali kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni 100 katika ujenzi na uboreshaji wa mifumo ya kisasa ya ukusanyaji wa kodi.

Bwana Mwenda amesema mfumo huo umeundwa kwa kuzingatia changamoto na malalamiko ya muda mrefu yaliyokuwa yakikabili walipa kodi, hususan katika masuala ya urahisi wa ulipaji, ufanisi wa huduma na uwazi katika makadirio na ukusanyaji wa kodi za ndani.

Ameeleza kuwa kupitia mfumo huo mpya, TRA inalenga kuongeza uwazi na uwajibikaji, kupunguza mwingiliano wa moja kwa moja kati ya mlipa kodi na mtumishi wa umma, pamoja na kuimarisha matumizi ya teknolojia katika kusimamia mapato ya Serikali.

Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu huyo, utekelezaji wa mfumo mpya wa ukusanyaji wa kodi utasaidia kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato, kuboresha mazingira ya biashara, na hatimaye kuchochea maendeleo ya Taifa kwa kuhakikisha rasilimali za Serikali zinapatikana kwa wakati na kwa uwiano unaostahili.


Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...