Na Said Mwishehe,Michuzi Blog
KAMPUNI ya Dorkin Organic Farming Co. Ltd ambayo imekuwa ikijihusika na tiba lishe kwa kutumia vyakula asili imezindua rasmi mgahawa wa chakula asili katika eneo la Gongolamboto wilayani Ilala Jijini Dar es Salaam.
Katika mgawa huo kutakuwa kunauzwa juisi,supu, ugali unaotokana na mahindi ya asili ambayo mbegu zake zimekuwepo tangu mwaka 1570 pamoja na uji wa maajabu unatokana na ndizi kitarasa na katika uji huo kuna faida mbalimbali ikiwemo ya madini muhimu yanayohitajika mwilini.
Pamoja na hayo imeelezwa uzinduzi wa mgahawa huo ni wa matumaini mapya ya afya, uchumi wa kilimo hai, na heshima ya Taifa la Tanzania katika sayansi ya chakula uponyaji.
Akizungumza leo Januari 28,2026 wakati wa uzinduzi wa Mgahawa huo wa chakula asili ,Mgeni rasmi ambaye ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Amana jijini Dar es Salaam Dk.Brayson Haule amesema kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi kula vyakula vya asili ili kuhakikisha wanakuwa na afya bora.
“Tunatoa rai wananchi wale vyakula vya asili ambavyo havina gharama kubwa na vinapatikana kwa urahisi hata kwa kulima wenyewe.Vyakula vya asili vinachangia kwa kiasi kikubwa pia ongezeko la damu mwilini kwani hivi sasa kumekuwa na changamoto kubwa ya upungufu wa damu kwa akina mama wajawazito,watoto na wazee .
Katika uzinduzi wa mgahawa huo wa vyakula vya asili,Dk.Haule amempongeza Profesa Dorcas Kibona kupitia kampuni yake ya Dorkin Organic Farming Co. Ltd kwa kuanzisha mgahawa wa vyakula vya asili katika eneo la Gongolamboto.
Aidha amesema Serikali inatambua umuhimu wa tiba asili na kwa sasa imeshaweka milango wazi kati ya sekta ya afya na tiba asili huku akitoa mfano kuna hospitali tano zimeteuliwa kuwa na vyakula na dawa asili na miongoni mwa hospitali hizo ni hospitali ya Temeke ambako kuna duka maalum kwa ajili ya vyakula na dawa asili ambazo zimethibishwa.
“Na kwa sasa Serikali inahamasisha matokeo na matumizi ya tafiti ambazo zimefanyika nchini, hivyo tunampongeza Profesa Dorcas kwa kuwa mfano wa kuigwa na maprofesa wengine kwani ameweza kufanya tafiti katika mazingira yetu na akaiweka vitendo.”
Kwa upande wake Profesa Dorcas Kibona ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Dorkin Organic Farming Co. Ltd inayojihusisha na utafiti wa vyakula vya asili vyenye uwezo wa kuponya na kuimarisha afya ya binadamu ametoa rai kwa Wizara ya Afya kuona haja ya kuendelea kutenga maeneo katika hospitali za umma kuwa na maeneo ambayo vyakula asili vitapatikana.
Aidha amesema “Tuko hapa kwa ajili ya afya na naomba nirudi nyuma kidogo kwenye kitabu cha Biblia tena Mwanzo Moja katika mstari wa 1-12 kuna mambo matano nataka nikupitishe pale kwanini ninafanya haya,cha kwanza nimeangalia aridhi , udongo,maji ,mbegu na mwisho nikaangalia afya
“Mungu wakati anaumba Dunia alimuumba mwanadamu lakini mwanadamu aliumbwa siku ya sita ya uumbaji .Vitu vyote viliumbwa mwanzo kabisa,Adam aliumbwa siku ya sita lakini baada ya kuumbwa alipewa bustani ambapo agizo alililopewa na Mungu ailinde na kuitunza na baada ya kuitunza atakutana na kila kitu kinachogitajiwa katika maisha yake
“Sasa sisi leo tumeikuta dunia imechupushwa katika njia yake katika eneo la kulima,kutunza. Lakini Dorkin Organic kwa kuangalia hilo tukachagua mambo matano.Kwanini magonjwa yamekuwa mengi,kwanini watu wanakufa kwa umri mdogo,nikajua shida ni afya na afya haitoki mbali inatoka kwenye aridhi
“Aridhi lazima iwe na udongo lakini tumeikuta haina rotuba kwani udongo umechoka sana, kuna kemikamili za viwandani zinachosha udongo na asili ya udongo kuna madini ya chokaa na yameshachukuliwa yote na dawa za viwandani.
“Dorkin Organic kwa kutambua tukafanya utafiti tukaona shida sio chakula kiwandani,shida sio chakula kwenye hotel,shida sio chakula kwa mama anayepika.Shida ni kule shambani tukajidhatiti vizuri tukaanza shambani
“Nimekuwa mtanzania wa kwanza kupima chakula cha kiasili katika maabara ya India nikiongozwa na Serikali yangu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Nadharia inasema homoni ya Iswilini inapatikana kwa wanyama peke yake ambao ni Kima na Nguruwe sasa mimi nakuja na homoni ya Iswilini kutoka kwenye tunda la ndizi kitarasa.”
Hata hivyo ameeema kuzinduliwa kwa mgahawa wa vyakula asilia ni muendelezo wa kuhakikisha jamii ya Watanzania inapata vyakula ambavyo vitawaepusha na magonjwa na mgahawa huo utakuwa wazi muda wote ili watu wapate uji wa maajabu, juisi ya maajaabu na supu ya maajabu inayotokana na vyakula vya asili.
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...