*Mkurugenzi Mtendaji amshukuru Rais Samia miradi 66 ikitelelezwa
Na Said Mwishehe,Michuzi Blog
HALMASHAURI ya Meru mkoani Arusha imetoa shukrani kwa Serikali chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambapo Halmashauri hiyo imetekeleza miradi 66.
Akizungumza wakati wa ziara ya waandishi wa habari waliotembelea miradi ya TASAF inayotekelezwa kupitia OPEC Fund Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwalimu Zainab Makwiya ametumia nafasi hiyo kuelezea kutekelezwa kwa moradi ya TASAF.
“Nawashukuru timu zima ya TASAF kwa kuendelea kutuamini Meru kwa kutupatia miradi ya maendeleo.Halmashauri yetu imekuwa ılığa ya vizuri katika kutekeleza miradi ya TASAF ikiwemo ya miradi ya OPEC.
“Pia niishukuru Serikali yangu inaongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuridhika haya yote yanayoendelea ndani ya Meru kwasababu hizi ni fedha zinazokuja kwa ajili ya miradi bila Rais kukubali huenda tusingepokea. Kwahiyo tunamshukuru na tunamuomba aendelee kututafutia zaidi ili tutekeleze miradi.
“Ninafahamu jinsi gani halmashauri zilizovyokuwa zinahangaika kutafuta fedha za miradi ya maendeleo hasa ikifika katika kipindi kama hiki cha watoto kwenda shule kidado cha kwanza , darasa la awali na darasa la kwanza.”
Amefafanua kwasasa mambo yamekuwa tofauti kwasababu fedha za halmashauri na washirika wengine TASAF imekuwa mkombozi mkubwa akitolea mfano katika halmashauri yake wanayo miradi mingi ya madarasa ambayo hapo awali wazazi walitakiwa wachangie au Mkurugenzi na mkuu wa wilaya watafute fedha lakini sasa hivi wanachokifanya ni kusimamia tu miradi ikamilike
“Ukiachana na hiyo watoto wa kike walikuwa wanapata shida hasa wale waliokuwa wanakaa mazingira magumu lakini kupitia TASAF wameweza kujenga mabweni ambayo sasa hawatembei tena umbali mrefu wako mabwenini wanapata huduma zote.
“Tukiachana na mabweni katika sekta ya afya tumejenga jengo la afya afya ya mama na mtoto katika Kituo cha afya Mbuguni na jengo limeanza kutumika.Kwahiyo tunashukuru TASAF kwa miradi ambayo imetuletea,”amesema Mwalimu Makwiya.
Ameongeza pia kupitia TASAF wamepata miradi ya nyumba za walimu ambapo kuna baadhi ya shule walimu walikuwa wanateseka yaani wanagawana vyumba ,mwalimu anakaa kwenye chumba kimoja kama amepanga kwani unakuta nyumba ya vyumba vitatu wanakaa walimu watatu.
“Lakini kwa sasa katika maeneo ambayo TASAF imetupatia mradi wa nyumba za walimu leo hii hata ukienda unafurahi maana walimu wanafanya kazi vizuri.
Aidha amesema Halmashauri ya Wilaya ya Meru kazi kubwa inayofanyika ni kilimo, ufugaji na biashara.”Katika kilimo tumepata miradi ya umwagiliaji ambapo sasa hivi tumeongeza uzalishaji,nikitoa mfano Ngabobo ni kwa wamasai lakini wanalima na wanazalisha nyanya na mbogamboga
“Kwa maana hiyo uzalishaji umeongezeka kwani wanapata fedha kupitia kupitia mifugo lakini pia kupitia kilimo na kwa Ngobobo TASAF kupitia mradi wa OPEC imejenga mifereji ambayo kwasasa maji yanakwenda mashambani na wakati huo huo kwa matumizi mengine ya kijamii.
“Hakika TASAF mmetukomboa ndani ya halmashauri ya Meru lakini sio kutukomboa tu mmeleta utulivu kwa familia kwasababu watu walikuwa wanakimbia majumbani.Tumetekeleza miradi ya TASAF kwa kiwango kikubwa hivyo wakati miradi ya TASAF inafika mwisho sisi tulishakamilisha miradi yote.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...